Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WALIMU WANASEMA NINI JUU YA MATOKEO MABAYA YA KIDATO CHA NNE.....HAPA WANAFUNGUKA.......




BAADA  ya waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Mh Shukuru Kawambwa kutangaza matokeo ya kidato cha nne 2012 ambapo matokeo hayo yalionesha idadi kubwa ya wanafunzi kufeli mtihani huo….Mengi yameongelewa 
juu ya matokeo hayo……..
Mashiho 150! Blog imeongea na baadhi ya walimu mbalimbali na wametoa sababu zao na maoni kwa masharti ya kutotaja majina yao….
Na hapa wanafunguka zaidi walimu hao…………..

Mwalimu 1
“Ok mfumo wa elimu hasa ngazi  ya uongozi kuanzia taifa mpaka ngazi ya chini hakuna anayehangaika na mafanikio ya watoto wote  wanawaza kupiga pesa kutoka kimaisha..mfanomaafisa elimu ngazi ya wilaya na mikoa wapo busy na maofisini na vikao hawajuimwalimu yupi yupo kituoni na yupi hayupo,yupi anafundisha nini na namna gani.Kwa wakuu wa shule ndo hata hawahangaikimtoto yupi anakuja shule na anafanya nini busy na capitation ujaua hata hela za kununuliavitabu wanazipiga!!Pilini maandalizi mabovu tunasajili watoto ambao tunajua kabisa hawawezi kufaulu sasa tunashangaa nini? Mtoto anatokashule ya msingi hajui kusoma na kuandika Kiswahili hivi atamudu masomo ya sekondari??MAONI::Wakuu wa shule wapewe mamlaka ya  kusimamia nidhamu mashuleni,wapewe uwezo wa kusajili wanafunzi wenye uwezo wa kufaulu tu.Uwekwe wastani  wa kufaulu kwa kila  kidato ili kila anayehamia  darasa Fulani awe amekidhi vigezo……”Mwalimu kutoka Tabora


Mwalimu 2
“Wanafunzi hawana nidhamu,hawasomi,utandawazi umewatawala,haki za wanafunzi zimezidi kuwatetetea mara adhabu kufutwa ona sasa mambo yanavyokuwa tunaiga mambo ya ulaya,mapenzi,mitaala mibovu,malipo kwa  walimu ,vitendea kazi duni,ushirikiano walimu na wazazi hakuna” Serikali ikae chini iangalie mzaha mzaha hutumbua usaha….Mwalimu kutoka Kilimanjaro
Mwalimu3
“Hivi kama mwajiri wako hakuthamini kwanza huwezi kufanya kazi kwa moyo,,,mimi nimepandishwa daraja kurekebishiwa mshahara inachukuwa muda kweli,ukisharekebishiwa unaclaim Arreas unazisotea mpaka sasa wala sijazipata,utakuwa na moyo kweli wa kuwafundisha wanafunzi kweli…..Halafu NECTA maswali wanayotoa kwenye mtihani yao yako nje ya kile kinachofundishwa shuleni….Kuanzisha shule nyingi kwa kukurupuka bila ya kuwa na vitendea kazi matokeo yake ndo haya….Hata hivyo sera ya elimu ya hapa nchini sio nzuri kwani inalazimisha kila mtu asome aende sekondari wakati wengine uwezo hawana…njia pia ya kuwatahini watoto wa darasa la saba ni hafifu sana kani maswali ya kuchagua hasa Hisabati hayawezi kumpima mwanafunzi uelewa wake…….Serikali kama haishtuki huu ni mwanzo tu…..Serikali itupe haki yetu tunayotaka waone kama  kazi haitafanyika…..Mwalimu kutoka Sumbawanga.

Mwalimu 4

Tuna wasiwasi  na software  wanazotumia kustandadize matokeo zilikuwa na mushkeli. Pili kuna wasiwasi  mkuu juu ya mahusiano ambayo yanaonekana si mazuri kati ya  waziri kawambwa na watendani wa baraza la mtihani kuna tatizo pale.Tatu mgogoro kati ya walimu na serikali na morali ya utendaji kazi kutokana na kipato kidogo hivyo kujishughulisha na  shughuli nyingine za kujiongezea kipato zaidi ya  ufundishaji.Lakini pia  hili laweza kuu.Watoto hawasomi kikamilifu.Wapo busy na facebook,ngono, headphonr kichwani muda  mwingi wakilisikiliza Diamond"Nataka Kulewa"..Na mitaala yetu mibovu mno na kubadilishwa kila mara bila mpango na weledi wa wizara zao,hivyo kutenda kazi bila ufanisi hasa  katika Wizara ya elimu.Watoto wa vigogo kusoma shule hizi za  St Kayumba .Yangu ni hayo....Mwalimu Kutoka Mbeya...


Mwalimu 5
Walimu tumepoteza morali ya kufundisha,madai ya walimu hayarimizwi,mtaala wa eelimu hapa nchini bado ni tatizo, hatuna mtaala rasmi,kila shule ila vitabu vyake vya kiada,wazazi haweasukumi watoto katika kusoma,mapenzi yamewatawala sana watoto siku hizi……..

USHAURI:: wazazi teache kuwa busy sana na kuawaacha watoto peke yao bila kuwafuatilia masuala ya shule,serikali iangalie upya masilahi ya walimu itupe teaching allowance mbona private wanalipwa vizuri wanafanya kazi kufa na kupona na ndo maana matokeo kule ni mazuri,kwanza walimu wengi wa serikali hawafundishi wanakimbila kufundisha ziada private kwenye maslahi. Watoto nao sasa waache mambo ya anasa kwenda club na sterehe nyingine hata kama dunia hii ni ya utandawazi……..Mimi ningekuwa Waziri ningekataza katakata mwanafunzi yeyote kuwa na simu ya mkononi mpaka amalize shule…….Mwalimu kutoka Mbozi Vwawa
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top