Baadhi ya wanafunzi hao wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha biashara hiyo ya ngono.
PENGINE haya tunaweza kuyaweka kwenye kundi la madhara yatokanayo na utandawazi. Mitandao ya kijamii ipo inayowasaidia wanafunzi katika masomo yao na kazi, lakini wengine wanatumia mitandao hiyo visivyo.
Uchunguzi wa Mwananchi
umebaini kuwa matumizi mabaya ya teknolojia hasa mitandao ya kijamii yamechochea
ongezeko la uhalifu, ubakaji, matumizi ya dawa za kulevya na zaidi biashara ya
ukahaba vyuoni.
Mitandao ya ‘Facebook’,
‘Twitter’, ‘BBM’, ‘Instagram’ inafahamika kwa namna inavyoweza kuwaunganisha
watu kutokana na urahisi wake katika kuitumia.
KWA HABARI ZA UDAKU, Tembelea www.shiladeux.blogspot.com
Mwananchi limebaini kuwa
katika mitandao hiyo makundi mbalimbali yameanzishwa yakiwa na malengo
tofauti.
Baadhi wameanzisha
makundi kwa lengo la kujenga mitandao ya kibishara, kidini, michezo, burudani,
vichekesho na mengine ambayo mara nyingi huwa wazi na yeyote anaweza kujiunga na
kuona kinachoendelea ndani.
Mbali na hayo ndani ya
mtandao wa ‘Facebook na ‘BBM’ yapo makundi yanayoendesha biashara ya ukahaba,
yakiwahusisha wanafunzi wa vyuo vikuu mbalimbali
nchini.
Uchunguzi umebaini kuwa
wanafunzi hao wanaofanya biashara ya ukahaba kwa kutumia mitandao wameweka picha
na namba kwa ajili ya mawasiliano kwa mteja atakayekubaliana na bei
waliyoweka.
Baadhi ya wanafunzi hao
wanatumia mtandao wa ‘University Tanzania Jokes’, ‘Jicho la Mvulana Liko Fasta
Kuliko Google’, ‘Benki ya Utamu Tanzania’ na nyingine katika kufanikisha
biashara hiyo ya ngono.
Ukiingia katika mitandao
ya Facebook, Twitter, BBM, Instagram, utabaini kuwapo kwa makundi yaliyoundwa
kutengeneza mitandao ya ngono, ambayo huweka pia namba za simu za wahusika,
zikiambatana na picha, ambao ikiwa utaangalia picha na kuvutiwa, unaweza ukapiga
simu husika kuzungumza naye kwa kufanya mapatano kabla ya
kukubaliana.
Uchunguzi wa Mwananchi Jumapili umebaini kuwa mwanamume anaweza kumpata msichana kutoka chuo kikuu chochote nchini anayefanya biashara ya ukahaba kupitia mitandao hiyo.
Baadhi ya vyuo
wanavyotoka wasichana wanaofanya biashara hiyo na kujitangaza kwenye mitandao ni
pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine (SAUT), Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) na
Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
Kwa nyakati tofauti,
waandishi wa gazeti la Mwananchi walitembelea makundi yanayojinadi kufanya
biashara hiyo pamoja na kufanya mawasiliano na wasichana watatu ambao waliweka
picha na namba zao kwenye mtandao.
Post a Comment