mashaka WATU wanaohoji kutokuwepo kwa hati halisi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar na kusema hati hiyo ipo na iwapo hawaamini wanaweza kwenda Umoja wa Mataifa New York.
Amesema Muungano wa Tanganyika na Zanzibar chimbuko la kuasisiwa kwake kulitokana na ridhaa ya wananchi wa pande mbili za Muungano na kuwataka wanaowababisha wananchi kwa maneno ya mitaani kuacha kufanya hivyo kwa sababu kila swali lao lina jawabu lake.
Dk Shein ambaye pia ni Makamo Mwenyeki wa CCM Zanzibar amesema kuundwa kwa Muungano halikuwa ni jambo la kubahatisha bali lina malengo yaliokusudiwa kabla ya kupatikana Uhuru ya Tanganyika mwaka 1961 na kufanyika kwa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar Januri 12,1964.
Amesema wenye wasiwasi na kutokuwepo kwa hati ya Muungano wamfuate ikulu awaonyeshe chumba walichokutana Mwalimu Julius Nyerere na Sheikh Abeid Karume na kufanya makubaliano ya mwisho kabla ya kuunganisha nchi zao
Ameeleza kuwa madhumuni ya vyama vya TANU na ASP yalilingana tokea vyama hivyo vikiwa katika harakati zake za kujikomboa hivyo kurahisisha hata kazi ya kuziunganisha nchi hizo mwaka 1964 pia vyama hivyo na kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977.
Aidha Makamo huyo Mwenyekiti wa CCM amewaeleza wananchi kuwa Mapinduzi ya Zanzibar ndiyo Uhuru kamili wa visiwa vya Unguja na Pemba huku akiwataka wananchi kutowasiliza watu wanaopotosha ukweli na kuwataka kuacha kufanya hivyo.
Dk Shein amesema watu wanaobeza ukweli huo hawana nguvu ya hoja bali wana lengo la kuwagawa wananchi ili waweze kuyafikia matarajio yao ambayo amesisitiza yanapaswa kupuuzwa na kila mpenda amani na umoja.
Amewataka watu hao kupuuzwa kwasababu hawajui wafanyalo na kwamba wanamangamanga ili kutaka kuwagawa wananchi bila ya kufikiri kwa makini .
Akizungumzia faida za Muungano Dk Shein amesema kiuhalisia wananchi wa Zanzibar ndiyo wanaofaidika na Muungano huo kwani kila uendepa katika Tamnzania Bara kuna wazanaziabri waliotamalaki na kuwekeza miradi na mitaji .
Alisema Zanzibar inafaidika na siko la Bara ambapo kabla ya Mapinduzi ilikuwa ikiagiza bidhaa za vyakula na mahitaji mengine kutoka nchi za Pakistan, Japan na mashariki ya mbali jambo ambalo sasa linapatikana kutoka Mikoa ya Bara
Kwa upnde wake Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai akizunguimza kabla ya kumkaribisha Dk Shein ,amesema nguvu ya umoja na maelewano kati ya visiwa vya Unguja na Pemba inatokana na kuwepo kwa Muungano na kusema nje ya jambo hilo lolote linaweza kutokea.
Vuai amesema Muungano wa Tanzania licha ya kuleta tija za kiuchumi lakini pia kwa kipindi chote cha miaka 49 ya kuwepo kwake umelinda na kusimamia usalama wa raia na mali zao.
Amesema hata pale Tanznia ilipovamiwa na majeshi ya Idd Amini mwaka 1978,wanajeshi wa Zanzibar waliingia vitani ili kuihami nchi yao vikiwemo visiwa vya Unguja na Pemba na kwamba nje ya Muungano umoja huo unaweza kuparaganyika .
Naibu huyo Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar,amesema CCM itaendelea kujivunia matunda ya TANU na ASP kutokana na kupigania kwao maslahi ya watu waliokuwa wakikandamizwa na kubaguliwa katika ardhi ya nchi zao.
Amesema vyama hivyo kwa pamoja vilihakikiisha vinajenga misingi imara ya heshama na utu kwa kila binadamu na kuondosha matabaka,ubaguzi wa rangi na maonevu hadi pale vilipoamua kuunganisha nguvu zake na kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi mwaka 1977.