Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZAZI MKOANI LINDI WATAKIWA KUSIMAMIA MAENDELEO YA ELIMU YA WATOTO WAO

 

IMG_6755
Wazazi mkoani Lindi wametakiwa kusimamia elimu ya watoto wao kwa kuhakikisha kuwa wanaenda shule, wanakagua madaftari yao na kuwarekebisha pale ambapo wamekosea kwa kufanya hivyo watafaulu vizuri katika masomo na kufanikiwa kimaisha kwani elimu ni msingi wa maendeleo.
Wito huo umetolewa jana na mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye kilele cha sherehe za maadhimisho ya miaka 36 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) zilizofanyika kimkoa katika kata ya Rondo wilaya ya Lindi vijijini.

Mama Kikwete ambaye pia ni Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM taifa toka wilaya ya Lindi mjini alisema kuwa maendeleo ya elimu si mazuri katika mkoa huo hivyo basi kina baba washirikiane na wake zao kuhakikisha kuwa watoto wanahudhuria shule na kufanya vizuri katika masomo yao.
“Ninyi watoto nawasihi msome kwa bidii mkumbuke kuwa huu si wakati wa mtoto kukatisha masomo kwa ajili ya kupata ujauzito kwani mkiwa na elimu kutakuwa na uhakika wa kupatikana kwa wataalamu mbalimbali katika mkoa huu na kutatua tatizo la kutokuwa na wataalamu ambalo limedumu kwa muda mrefu”, alisema Mama Kikwete.
Aidha Mjumbe huyo wa Halmashauri kuu ya CCM taifa aliwataka wanawake kutosubiri nafasi za upendeleo za viti maalum bali wagombee nafasi mbalimbali za uongozi ndani na nje ya chama ili wafike katika ngazi ya maamuzi na kuachana na fikira kuwa wao hawawezi kumwaga sera wakati wa uchaguzi.
Alimalizia kwa kuwataka wakazi wa mkoa huo kudumisha amani, upendo na utulivu, kufanya kazi kwa bidiii, maarifa na kujituma, wakulima walime kilimo cha kisasa ambacho kitawafanya wavune mazao mengi zaidi pia wafanyakazi watumie muda wa kazi kufanya kazi na kuwahudumia wananchi.
Mama Kikwete pia alifungua jengo la ofisi ya CCM lenye thamani ya shilingi milioni 35 ambalo limejengwa na Mbunge wa jimbo la Mtama ambaye ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Benard Membe.
Waziri Membe alisema kuwa jengo hilo lina vyumba sita ambavyo ni ofisi za jumuia zote za chama hicho ambazo ni Vijana, Wanawake, Wazazi, pia kuna ofisi za Mbunge, Mjumbe wa NEC na chumba cha mikutano.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Ally Mtupa aliwataka wanachama wa chama hicho kuwa na mahusiano mazuri baina yao na viongozi wanaowaongoza. Wakisikia jambo wasiwe na papara ya kukimbilia kuandamana bali wafanye upelelezi kwanza na wakishabaini ukweli ndipo wachukue hatua.
Mtupa alisema, “Hivi sasa kuna watu wanapita mitaani na kupotosha ukweli kuwa Serikali yetu haijaleta maendeleo, wamesahau kuwa wanatembea katika barabara na kutibiwa katika Hospitali zilizojenga na CCM, tunawaomba watu hawa wawaheshimu viongozi wanaotawala kwani hata vitabu vya dini vinasisitiza umuhimu wa kuwatii viongozi waliopewa mamlaka ya kutawala”.
Sherehe hizo zilienda sambamba na mchango wa matembezi ya mshikamono ambapo zaidi ya shilingi milioni mbili zilipatikana, ufunguzi wa ofisi za CCM, ufanyaji wa usafi wa mazingira , kuwatembelea wagonjwa mahospitalini, utoaji wa kadi kwa wanachama wapya ambapo wanachama wa kawaida 286 , jumuia ya wazazi 63 na kutoka vyama vya upinzani 23 walipewa kadi.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top