Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Fereji akitoa nasaha kwa Wazazi wa watoto wenye ulemavu kuwapa haki zinazostahiki katika hafla ya kukabidhi msaada kwa watu hao uliotolewa na Jumuiya ya Wazanzibari waishio nchini Canada katika Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar Weles. 
Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada (ZANCANA) Bishara Al Masroori akizungumza na Wazazi wa watoto wenye ulemavu (hawapo pichani) katika hafla ya kukabidhi msaada kwa watu hao. Kushoto ni Waziri wa Nch, Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Fereji Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar Weles.

Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Fereji akiwa na Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada Bishara Al Masroori wakimkadhi baiskeli ya walemavu Mtumwa Hamadi Khamis mkaazi wa Tomondo huko Weles Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar.
Mwakilishi wa Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada  (ZANCANA) Bishara Al Masroori akiwa na Mtoto mlemavu Amur Yunus Hamadi aliyebebwa na Baba yake akiwa na mdoli wa kuchezea huko Weles Makao Makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar.  Picha na (Makame Mshenga-Maelezo Zanzibar).
Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa kwanza wa Rais Fatuma Abdullhabibu Fereji amesema kuna kila sababu za kuwasaidia Vipando watu wenye ulemavu ili waweze kufikia katika Shughuli zao na kuungana na wenzao katika harakati za maisha.Amesema hayo katika Makao makuu ya Jumuiya ya watu wenye ulemavu Zanzibar, Welesi alipokuwa akikabidhi Baskeli za kutembelea na vifaa mbali mbali kwa Watoto wenye ulemavu, ukiwa ni msada kutoka Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Canada (ZANCANA).
Amesema msaada wa Jumuiya ya ZANCANA unafaa kuigwa na kupigiwa mfano kwani utawawezesha Walemavu hao kukabiliana na majukumu yao ya kila siku kwa wepesi.
Waziri Fereji amesema Walemavu wanahitaji kufanya mambo mengi ya msingi lakini kuna wakati hushindwa kutokana na ukosefu wa usafiri ikiwa ni pamoja na Baskeli na vifaa vingine vinavyoweza kuwasaidia kufanya mambo yao ipasavyo.
Amesema mpaka hivi leo kuna baadhi ya Wazazi wanawafungia ndani walemavu na kuwakosesha haki zao za msingi kwa madai kuwa hawataweza kufikia masafa ambayo huduma zinatolewa.
Jumuiya ya Wazanzibari wanaoishi nchini Kanada (ZANCANA) imetoa msaada kwa Watu wenye ulemavu ikiwa ni pamoja na Baiskeli za kutembelea, Viti, vifaa vya watoto vya kuchezea ikiwa ni jitihada za kusaidia ndugu zao wanaoishi katika mazingira magumu .
IMETOLEWA NA MAELEZO ZANZIBAR