|
Waziri
Kagasheki
***************
Waziri wa
Maliasili na Utalii Mheshimiwa Khamis Suedi Kagasheki amewaruhusu watu 292 ambao
vibali vyao vilisitishwa mwezi Januari mwaka huu, kutokana na utata
uliojitokeza, kuendelea na uvunaji katika Shamba la Sao Hill. Waziri Kagasheki
ametoa ruhusa hiyo baada ya kujiridhisha kuwa watu hao walipata vibali hivyo kwa
kufuata taratibu za uvunaji.
Mheshimiwa
Kagasheki wakati alipotembelea Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa tarehe 25 na 26
Januari 2013 ili kusikiliza kero zilizopo Wilayani humo kuhusiana na Shamba la
miti la Sao Hill, aliahidi kufanyia kazi baadhi ya masuala
yaliyojitokeza.
Kuhusu
suala la vibali 292 vilivyotolewa katika msimu wa mwaka 2012/13 na kusitishwa
wakati wa ziara yake, Waziri Kagasheki amelifanyia kazi na kubaini kuwa matatizo
na changamoto zilizojitokeza zilitokana na utendaji katika kipindi cha mpito,
hususan mabadiliko ya utaratibu wa utoaji vibali vya uvunaji.
Hivyo,
wadau hao 292 ambao hawana vibali rasmi vilivyochapishwa kutokana na kutumika
utaratibu wa zamani, wameruhusiwa kukamilisha taratibu na kupewa vibali rasmi
vya uvunaji.
Ruhusa
hii inawahusu wavunaji wote waliofuata taratibu zote za usajili, ikiwa ni pamoja
na kupata usajili na kulipia maduhuli na tozo mbalimbali za Serikali ambavyo
ndivyo vigezo muhimu vya kumfanya mvunaji kufanya shughuli zake zinazohusiana na
masuala yote ya uvunaji.
Wizara ya
Maliasili na utalii inaendelea kufanyia kazi kero zote zilizojitokeza wakati wa
ziara hiyo Waziri na taarifa itaendelea kutolewa kuhusu utekelezaji
wake.
[MWISHO]
George
Matiko
MSEMAJI
WIZARA YA
MALIASILI NA UTALII
Tarehe 21
Februari,
2013
|
on Thursday, February 21, 2013
Post a Comment