Mhe. Membe akipitia Itifaki hiyo kabla ya kusainiwa
huku Bw. John M. Haule, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa akishuhudia.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
Mhe. Bernard K. Membe (Mb.), akiweka saini Itifaki ya Amani na Usalama ya Nchi
za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC). Uwekaji saini huo ulifanyika katika Hoteli
ya New Africa, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Membe akifafanua jambo baada ya shughuli ya
utiaji saini kukamilika.
Mhe. Membe akijadiliana jambo na Katibu Mkuu wake Bw.
Haule. Mwingine katika picha ni Mhe. Pereira Ame Silima (Mb.), Naibu Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Dkt.
Richard Sezibera (kulia) akijadiliana jambo na Waziri wa Ulinzi wa
Uganda.
Mhe. Membe (wa pili kushoto) akiwa na viongozi wenzake
wa nchi za EAC wakiwa wameshikilia Itifaki hiyo mara baada ya
kusainiwa
Mhe. Membe akifanya mahojiano na Waandishi wa Habari
baada ya shughuli ya utiaji saini kukamilika.Picha zote na Wizara ya Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Post a Comment