Mark Simmonds, Waziri wa Uingereza anayeshughulikia
masuala ya Afrika, Jumuiya ya Madola na Nchi za Kigeni.
Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo
---
imeandaliwa na Kuletwa hapa kutoka nchini uingereza na Freddy Macha
Waziri wa Nishati na Umeme, Profesa Sospeter Muhongo
anamewasili Uingereza leo kwa ziara ya siku nne.
Waziri alipokewa na Balozi wetu mheshimiwa Peter
Kallaghe na anatazamiwa kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali
ya Uingereza na wataalamu wanaohusiana na shughuli za madini, maendeleo
na kimataifa.
Miongoni mwa maofisa anaotazamiwa kukutana nao kesho
Jumatatu ni pamoja na Waziri wa Uingereza anayeshughulikia masuala
ya Kiafrika, Jumuiya ya Madola na nchi za Kigeni, Bwana Mark Simmonds;
Naibu Waziri wa Maendeleo ya Kimataifa Uingereza, Bi Lynne Featherstone
na Mbunge wa Stratford chama cha Conservative, Jeremy Leffroy
ambaye pia ni mwenyekiti wa kundi la Wabunge wa Uingereza wanaoshughulikia
Tanzania (APPG).
Jumanne saa kumi na moja jioni Waziri ambaye pia
ni Mbunge wa kuteuliwa amepanga kuongea na Watanzania wanaoishi Uingereza
ukumbi wa Ubalozi wetu London. Ukumbi uko 3 Stratford Place, London
W1C 1AS. Stratford Place iliyojishika na barabara kuu ya Bond- ni sekunde
chache tu mbele ya kituo cha magari moshi na mabasi cha Bond Street.
Waziri ambaye pia ni Mbunge wa kuteuliwa anaongozana
na Dk Athanas Macheyeki wa Ukaguzi wa Madini Tanzania, Seleman Hatibu
Chombo wa idara ya Nishati katika Wizara ya Madini na Nishati na Bwana
Sosthenes Masau Bigambo Massola, katibu wake muhtasi.
Waziri Muhongo ni msomi aliyebobea ndani ya
masuala ya kisayansi na taaluma ya mawe na madini. Mbali na kuwa profesa
na mhariri wa jarida la “Journal of African Journal Sciences” ni
vile vile mwanachama wa jumuiya mbalimbali za madini na sayansi
za kimataifa. Jumuiya hizo ni “Geological Society of London,” “Geological
Society of America,” “Chinese Academy of Geological Sciences”
na “Tanzania Academy of Sciences.”
Kiongozi huyu ni Makamu Rais wa Tume ya Tume ya
Ramani ya Madini duniani iliyoundwa 1881 Ufaransa. Lengo la tume hii
ni kuendeleza masuala ya mazingira, madini na hali ya hewa ya ulimwengu
na Rais wake ni Philippe Rossi.
Mshindi wa tuzo kadhaa za kielimu na kisayansi, Profesa
Muhongo alizaliwa Musoma mwaka 1954 akamaliza masomo yake vyuo vya Dar
es Salaam na Ujerumani. Mwaka juzi alizawadiwa “Ordre des Palmes Academiques”
ya serikali ya Ufaransa – inayotolewa kwa wataalamu waliochangia masuala
ya kielimu na kitamaduni toka lipoanzishwa na Mfalme maarufu Napoelon
karne ya 19.
Tovuti: www.freddymacha.com
Post a Comment