 |
| Hali
ilivyokuwa hii leo mara baada ya kivuko hicho kurejea
kazini. |
WAZIRI wa Uchukuzi
Dkt..Harrison Mwakyembe ameagiza kivuko cha Mv.Sammar III kiendelee kutoa huduma
ya usafiri ndani ya eneo la Bandari ya Mwanza Kaskazini linalomilikiwa na
Mamlaka ya Bandari nchini TPA.
Agizo hilo la Waziri
Mwakyembe limefuta uamuzi wa Uongozi wa Mamlaka ya Bandari PTA nchini na
kumaliza utata wa jambo hilo uliokuwa umezua sitofahamu na hata kutofautiana na
agizo la Kamati ya Ulinzi na Usalama la Mkoa wa Mwanza la kukiruhusu Kivuko cha
Sammar III kuendelea kutoa huduma katika eneo hilo la Mamlaka ya Bandari ya
Mwanza Kaskazini Jijini Mwanza.
Hatua hiyo inafuatia agizo la barua iliyotolewa kutoka kwa
Uongozi wa Mamlaka ya Bandari (PTA) waliyomwandikia na kumkabidhi Mwekezaji na
Mkurugenzi wa Kivuko cha MV.Sammar III Salum Ally yenye kumbukumbu NaMN/2/3/04
ya Januari 29 mwaka huu iliyosainiwa na Kaimu Mkuu wa Bandari (TPA) Mwanza
Richard Msechu,ambapo ilieleza kwamba agizo hilo limetoka na Wizara ya
Uchukuzi.
Agizo hilo lilionekana
kupingana na lile la Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa wa Mwanza lililoridhia
Kivuko hicho cha MV.Sammar III kuendelee kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria
na magari kati ya Mwanza na Kamanga Wilayani Sengerema ndani ya eneo la Mamlaka
ya Bandari ya Mwanza Kaskazini baada ya tamko la awali la Naibu Waziri wa
Uchukuzi Dr.Charles Tizeba alilolitoa Desemba 9 mwaka 2012 la kutaka Mamlaka
hiyo imuondoe eneo hilo na kumhamishia sehemu
nyingine.
 |
| Mbunge
mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki Fortunatus Masha
(UDP) |
Baada ya taarifa za
kuruhusiwa kuendelea na shughuli za kutoa huduma ya usafirishaji wa abiria na
magari, mamia ya wananchi na baadhi ya abiria wanaotumia kivuko cha Sammar III
wakiongozwa na Mbunge mstaafu wa Bunge la Afrika Mashariki Fortunatus Masha
(UDP) alisema kwamba uamuzi huo ni bubusara na ni mfano wa kuigwa kwa viongozi
wengine katika kuwatumikia wananchi kwa kuzingatia masilahi ya
umma.
Aidha alipongeza uamuzi
wa Waziri Dr. Mwakyembe umeonyesha kuwa ni mungwana na mtu anayejali sana na
hata pengine kuondoa kero za wananchi na kuwajali zaidi badala ya kuangalia
masilahi binafisi kama ilivyo kwa viongozi wengine ambao husababisha hata
wananchi kuwachukia na kuilaumu serikali yao iliyopo
madarakani.
Wananchi wa Jiji la
Mwanza na Kamanga Wilaya ya Sengerema leo asubuhi wamedhuru eneo la kamanga
wakiwa na mabango yenye ujumbe tofauti ya kuwapongeza Waziri Dkt.Mwakyembe, Mkuu
wa Mkoa Injinia Ndikilo na Kamati yake na Mbunge wa Jimbo la Sengerema William
Ngeleja kwa kusimamia na kuondosha kero hiyo kwa kukiruhusu Kivuko cha Sammar
III kuendelea kutoa huduma ya usafiri.
Mwenyekiti akizungumza
kushukuru sakata hilo kumalizika...
Mama Ester ambaye ni
mfanyabiashara ya chakula eneo hilo aliwakilisha akina mama kuzungumzia
kumalizika kwa sakata hilo..
 |
| Akina
mamalishe nashughuli zao za kipato eneo la Kamanga upande wa Sengerema leo
wameendelea na shughuli zao kama kawaida mara baada ya kusitisha zoezi hilo kwa
muda wa siku kadhaa wakati kivuko hicho kikiwa kwenye
katazo. |
 |
| Wananchi
wa Kamanga Wilaya ya Sengerema na bango
lao. |
 |
| Mkurugenzi
wa Kivuko cha Sammar III, Salum
Ally |
Kwa upande wake
Mkurugenzi wa Kivuko cha Sammar III, Salum Ally alisema kwamba anaupokea uamuzi
huo wa Waziri kwa mikono miwili, kwa vile ni uamuzi ambao umezingatia kero na
adha ambayo wangelipata wananchi lakini pia naye kama mwekezaji kwakuwa alitumia
gharama kubwa kuwekeza ikiwemo miundombinu ya eneo la kivuko pande zote mbili
Mwanza na Kamanga.
Post a Comment