Mechi namba 119 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Februari 13 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Yanga kuibuka ushindi wa mabao 4-0 imeingiza sh. milioni 68,438,000.
Watazamaji
12,147 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo iliyochezwa kwa viingilio
vya sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu
ikipata mgawo wa sh. 16,170,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani
(VAT) iliyolipwa ni sh. 10,439,694.92.
Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo 10,982 walikata tiketi hizo na kuingiza sh. 54,910,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 8,222,162.26,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 4,933,297.36, Kamati ya Ligi
sh.
4,933,297.36, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,466,648.68 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam(DRFA) sh. 1,918,504.53.
Post a Comment