TIMU
ya Azam Fc, ya jijini Dar es Salaam, ambao ni wawakilishi wa Tanzania
katika michuano ya Kombe la Shirikisho (CAF), leo tena imeeilambisha
Al-Nasri ya Sudan jumla ya Ice Cream 5-0, katika mchezo wao wa marudiano
uliochezwa leo katika Uwanja wa Juba, Sudan ya Kusini.
Katika
mchezo wa awali uliopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam,
Azam waliilaza timu hiyo kwa mabao 3-1, ambapo sasa Azam imefanikiwa
kusonga mbele katika katika michuano hiyo kwa kuibanjua jumla ya mabao
8-1 timu hiyo.
Credits: Sufiani Mafoto
Post a Comment