Mshauri wa Utamaduni
wa Ubalozi wa Jamhuri ya watu wa China kwa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Liu
Dong akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu manufaa ya
ujio wa Rais wa China, hali ya mkutano wa kwanza wa Bunge la umma ya 12 la
China pamoja na mkutano wa kwanza wa Baraza la mashauriano ya kisiasa la awamu
ya 12 la China. Pia China imeishukuru serikali ya Tanzania kwa mapokezi mazuri
wakati wa ziara ya Rais mpya XI Jinping ya Jamhuri ya Watu wa China, pamoja
na waandishi wa habari katika juhudi zakuendeleza uhusiano mzuri baina ya China
na Tanzania.
(Picha zote na Mwanakombo
Jumaa-MAELEZO).


Post a Comment