Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles
Kimei (kushoto), Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu na Balozi wa
China hapa nchini, Lü Youqing wakiwasili katika hoteli ya
Serena.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk.Charles
Kimei akitoa hotuba yake wakati wa uzinduzi huo.
Balozi wa China hapa nchini, Lü Youqing akitoa hotuba
yake.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji na
Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu akizungumza katika hafla hiyo.
DAR ES SALAAM,
Tanzania
MKURUGENZI Mtendaji wa Benki
ya CRDB, Dk.Charles Kimei, amewataka wajasiriamali na wawekezaji wanaofanya
biashara zao kati ya Tanzania na China, kuchangamkia fursa pana ya ukuzaji
mitaji yao na pato kwa kutumia huduma mpya ya CRDB China
Desk.
Dk Kimei aliyasema hayo jana
wakati wa hafla ya uzinduzi wa China Desk, inayotolewa na CRDB, itakayo
wahudumia wafanyabiashara, wajasiriamali na wawekezaji wanaofanyakazi zao baina
ya mataifa hayo rafiki.
“China Desk, ni huduma yenye
fursa inayoweza sio tu kusaidia kukuza mitaji na kutanua wigo wa maendeleo, bali
kudumisha ushirikiano wa kiuchumi na maendeleo baina ya China na Tanzania, ambao
uliasisiwa karibia nusu karne iliyopita,” alisema Dk Kimei katika hafla
hiyo.
Aidha, akizungumza katika
hafla hiyo iliyofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini, Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Uwekezaji na Uwezeshaji, Dk. Mary Nagu, aliiomba CRDB kuboresha
utoaji wa mikopo ya riba nafuu kwa wajasiriamali wadogo na wa kati, ili
kuharakisha ukuaji wa pato la Mtanzania na Taifa kwa
ujumla.
Dk Nagu alibainisha kuwa,
taasisi za kipesa nchini zina mchango mkubwa kuwawezesha wajasiriamali wadogo na
wa kati kukuza pato lao, kama zitakuwa tayari kuwapa mikopo yenye masharti nafuu
na riba ndogo, ili kusaidia harakati zao za kujikwamua na kukuza uchumi wa
taifa.
“CRDB mnastahili pongezi kwa
huduma hii, inayokuja wakati ambao Tanzania kama Taifa, lilimpokea rais mpya wa
China, Xi Jinping katika ziara ya kikazi. Taasisi nyingine za kifedha zitambue
umuhimu wa ushirikiano baina ya mataifa haya na kubuni huduma kama hizi,”
alisema Dk Nagu.
Aliongeza kwamba, kwa kuwa
harakati za kumkomboa Mtanzania zimeshika kasi, huku China ikijitoa kadri
iwezavyo kuisaidia Tanzania, kuna haja huduma kama hizo za China Desk
zikaambatana na mikakati endelevu ya kimandeleo, na taasisi nyingine nazo
zinastahili kuiga.
Kwa upande wake, Balozi wa
China hapa nchini, Lü Youqing, aliipongeza CRDB kwa kufuata nyayo za waasisi wa
China na Tanzania, kiasi cha kubuni na kuzindua China Desk – dawati
litakalowanufaisha wajasiriamali na wafanyabiara wa kila
upande.
“Huduma hii ni harakati
chanya inayofuata nyayo za waasisi wa ushirikiano baina ya China, Rais Mao Tse
Tung na Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere. Vizazi na vizazi vitabaki kujivunia na
kila mmoja atajisikia yu nyumbani anapokuwa katika moja ya nchi hizo,”
alisisitiza Youqing.
Credits: Habari Mseto Blog
Post a Comment