Akizungumza
jana, Lema alisema ameamua kuandaa maandamano hayo ya kudai maji kwani kwa zaidi
ya miezi sita sasa asilimia 70 ya wakazi wa Jiji la Arusha hawapati maji
safi.
“Nimewaandikia barua
AUWSA wiki mbili sasa nikiwataka wanipe mipango yao ya muda mfupi na mrefu ya
kuondoa tatizo la maji Arusha, kwani mimi kama mbunge ninaweza kushirikiana nao
kupunguza tatizo hili, lakini hawajajibu sasa tutawashinikiza kwa nguvu wa
umma,” alisema Lema.
Hata hivyo, Mkurugenzi
Mkuu wa AUWSA, Mhandisi Ruth Koya hakupatikana kuelezea kama amepokea barua hiyo
baada ya kutopatikana ofisini, pia simu yake ya mkononi ilikuwa
haipatikani.
Post a Comment