Hii leo wakenya wamepiga kura katika uchaguzi wa
kihistoria chini ya katiba mpya. Foleni tayari zimeanza kushuhudiwa katika
vituo.
Kinyang'anyiro
ni kikali kati ya Muungano wa Cord na Jubilee wa Raila Odinga
na Uhuru Kenyatta.
18:22: Mwandishi wa BBC
Jamuhuri Mwavyombo amesema kuwa kulika na matatu tofauti, mjini
Mombasa ambko kundi la MRC linaendesha harakati zake. Mashambulio y mawili,
yalifanyika mtaa wa Changamwe, ambako polisi walishambuliwa na tukio la tatu
katika kituo cha polisi eneo la Chumani Kilifi.
16:27
:Sehemu nyingi za starehe na ulevi mjini Nyeri Mkoa wa Kati zimefungwa
na zitafunguliwa Jumanne ili kuwaruhusu wapiga kura kupiga kura. Eneo la Mkoa wa
Kati lina tatizo la uraibu wa pombe
16:24:
Ng'endo Angela ambaye yuko Mooa wa Kati ansema kuwa
kuwa sababu ya hitilafi za kimitambo, tume imalzimika kutumia mfumo wa kawaida
kwa kutumia daftari za wapiga kura. Ni Nyeri peke yake ambako shughuli hiyo
ilifanikiwa kwa njia ya Elktroniki
15:54
Mwandishi wa BBC Emmanuel Igunza anasema kuwa foleni
mjini Nakuru zimeanza kupungua na huenda wapiga kura wakamaliza shughuli hiyo
itimiapo saa kumi na moja jioni muda wa mwisho wa kupiga kura
15:16
Mmoja wa wagombea wakuu wa urais Uhuru Kenyatta
ameelezea maskitiko yake kuhusu yaliyojiri Mombasa ambako washukiwa wa kundi la
MRC waliwaua polisi na raia katika mashambulizi usiku wa kuamkia leo. Lengo lao
lilikuwa kuvuruga shughuli ya uchaguzi
14:57
Mwandishi wa BBC mjini Kisumu Ann Mawathe anasema
milolongo ya watu imepungua sana katika sehemu nyingi za mji huo ikizingatiwa
kuwa asubuhi watu walikuwa wamejaa pomoni
14:51 Kuna taarifa kuwa magari ya
Abiria yameanza kuongeza nauli ya magari kwa sababu ya upungufu wa magari hayo
wakati wakenya wakiwa wamejitokeza kupiga kura
13:33
Tume ya uchaguzi imeagiza uachaguzi kurejelewa katika wodi tano kati ya
zote 1'450 ambako mitambo ya tume hiyo ilikumbwa na hitilafu pamoja na makosa
kwenye karatasi za kupigia kura
13:31 Katika baadhi ya vituo vya
kupigia kura, ambako foleni ndefu zimeshuhudiwa, taarifa zinasema kuwa watu
wanaonekana kukata tamaa na wameamua kurejea nyumbani kwani foleni
hazisongi
13:24 Mwandishi wa BBC Wanyama
wa Chebusire anaripoti kuwa gari la mbunge mmoja wa zamani
limeteketezwa moto katika kaunti ya Kakamega na watu wanaoaminika kuwa wafuasi
wa mpinzani wake.
11:25
Mkuu wa Polisi David Kimaiyo asema kuwa takriban
wanachama 200 wa kundi la MRC au Mombasa Republican Council walivamia kituo cha
polisi wa doria wakiwa wanaelekea kusambaratisha shughuli za kupiga
kura. Inaarifiwa polisi wanne waliuawa katika makabiliano kati
yao na wanachama hao.
11:14 Mgombea wa urais Uhuru
Kenyatta anapiga kura yake katika eneo bunge lake la Gatundu , mkoa wa
Kati
10:39
Mwandishi wa BBC aliye mjiniNyeri Ng'endo Angela anasema kila baada ya
nyumba kumi kuna kituo cha kupigia kura, wapiga kura wamejitokeza kwa wingi,
baadhi ya mashine za tume ya uchaguzi zilifeli lakini baada ya kushughulikiwa
mambo yakarejea kuwa sawa.
10:31 Mwandishi wa BBC mjini Eldoret
Wanyama wa Chebusire vituo vilifungua mapema mambo, yameenda
shwari kwa ujumla wake, lakini katika baadhi ya vituo, kumekuwa na mushkil ,
mashine ziligoma katika kituo cha kupigia kura cha shule ya msingi ya UG, zaidi
ya wapiga kura elfu tatu , hadi sasa ni chini ya watu hamsini wamepiga
10:27 Mkuu wa tume huru ya uchaguzi
Isaac Hassan anahutubia waandishi wa habari kuhusu changamoto
inazokabiliwa nazo tume hiyo. Isaac anasema vituo vilivyofungua kuchelewa,
vitahakikisha wapiga kura wote wamepiga kura
10:22: Ingawaje tume ya uchaguzi IEBC
inawakubalia watu wawasindikize wazee au wagonjwa kupiga kura, wapigaji kura
wengine wanawakataza kufanya hivyo. Mjini Kisumu katika kituo cha upigaji kura
cha Ukumbi wa Aga Khan, mwandishi wetu Ann Mawathe dada mmoja
alieyejipandikiza blanketi tumboni ili kuwahadaa watu na akubaliwe kwenda hadi
mwanzo wa foleni, alikatazwa kufanya hivyo na wapiga kura wenzake.
Katika kituo
hicho hicho, baba fulani aliyekuwa amebeba kipochi cha mkewe aliyekuwa na mtoto
mgongoni, naye alirudishwa hadi nyuma kabisa ya foleni hiyo. Pia, mwanamume
mwingine aliyejitwika ufahari fulani kwa vile alikuwa kavalia suti, na kutaka
kuruka foleni, alikatazwa kufanya hivyo.
09:04 Waziri mkuu Raila
Odinga ambaye pia anagombea urais amepiga kura yake katika eneo la
Kibera. Amesema licha ya kupata habari za baadhi ya vituo vya kupigia kura kuwa
na hitilafu kidogo, wapiga kura wasiwe na wasiwasi kwani mambo yatakuwa shwari
08:43 Mgombea wa urais wa muungano wa
CORD, waiziri mkuu Raila Odinga anatarajiwa kupiga kura yake
wakati wowote kuanzia sasa
08:30 Solomon Mugera
anasema kwamba kupiga kura kunachukua takriban dakika 12
08:25
Hassan Majid pia mwandishi wa BBC anasema kuwa polisi wamepata
mwili mmoja wa mtu aliyeuawa na mwingine kujeruhiwa kwa kukatwa panga katika
eneo la Mishomoroni
08:24 Mwandishi wa BBC mjini Mombasa,
Karen Allen anasema kuwa polisi wamepata maiti za polisi wanne
ambao wameuawa katika eneo la eneo la Changamwe , Kaskazini mwa Mombasa. Hana
taarifa zaidi kwa sasa
08:16:Frawaso Kimutai kupitia Bofya facebook yuko katika
kituo cha Menengai mjini Nakuru kura ilianza kupigwa saa moja asubuhi na foleni
ni ndefu ingawa inakwenda polepole mwendo wa kobe
08:15:Fatma Sanbur
yuko mtaani Kibera na anasema watu ni wengi sana lakini hakuna mbinu ya kupanga
foleni. Anasema watu wanapangwa kwa orodha ya majina na hata baada ya saa moja
tangu waanza kupangga foleni saa kumi na moja, shughuli ya upigaji kura ilikuwa
haijaanza
07:11James Mwangi:
Kwenye ukurasa wa Bofya Facebook wa Bofya bbcswahili anasema
yuko kwenye foleni na habanduki
07:14 Hison Nyakundi
: Yuko mjini Eldoret kwa Foleni tayari kupiga kura Bofya bbcswahili
07:24
Kips Oscar: Kupitia Bofya Facebook yuko katika
kaunti ya Marsabit anasema upigaji kura unaendelea bila wasiwasi na kuwa
wanatarajia shughuli itakamilika kwa muda bila wasiwasi
07:28: Mgombea mwenza wa Uhuru
Kenyatta, William Ruro amepiga kura mjini Eldoret
07:32:
William Ruto anasema kuwa anajivunia uchaguzi wa Kenya unafanyika kwa
amani licha ya dukuduku la wengi. Anasema anawataka wapinzani kukubali matokeo
ya uchaguzi vyovyote matokeo hayo yatakavyokuwa.
07:43 Upiga kura
bado haujaanza katika baadhi ya sehemu za Kenya. Wapiga kura wanalalamika kuwa
katika vituo kadhaa tarakilishi zimegoma na kwa hivyo watasubiri muda kabla ya
kupiga kura zao
07:47Eco Seyar Papa
akiwa mjini Nairobi anasema Wakenya wamejitokeza kwawingi jijini Nairobi katika
eneo la Dagoreti. Foleni zilianza kupigwa kuanzia saa tisa usiku tangu
kuanzishwa kwa demokirasia ncini Kenya watu waeneo hili hawajawai kujitokeza kwa
mapenzi kama inavyo onekana.
07:50 Mwandishi wa BBC Ann
Mawathe yuko mjini Kisumu na anasema ameona foleni ndefu sana watu
wakiwa hamasa kupiga kura. Wamepiga foleni tangu saa nane usiku.
07:52 Mombasa eneo la Kaloleni mpiga
kura mmoja amesema hadi kufikia sasa upigaji kura haujaanza kwani maafisa wa
tume ya uchaguzi bado hawajawasili na vifaa vyao
Post a Comment