Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

IGP SAIDI MWEMA AELEZEA SAKATA LA DK ULIMBOKA, KIBANDA.


 

IGP SAIDI MWEMA.
Dk Ulimboka kabla hajaanza kutibiwa.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda.




MKUU wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema amesema upelelezi wa kesi ya kutekwa, kuteswa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka bado haujakamilika.

Mbali na Dk. Ulimboka, IGP alisema kesi nyingine zote za aina hiyo pamoja na za mauaji ya watu mbalimbali, akiwemo Padri wa Kanisa Katoliki la Minara Miwili lililopo Mji Mkongwe Zanzibar, Evaristus Mushi (56), uchunguzi wake unaendelea.

IGP Mwema, aliyasema hayo jana wakati wa semina ya wakuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC), Mjini Dar es Salaam jana.

Dk. Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari Tanzania, alitekwa usiku wa kuamkia Juni 27, 2012.

Hata hivyo, suala hilo lilizua sintofahamu ya aina yake baada ya mtuhumiwa Joshua Mulundi, raia wa Kenya kukamatwa na kufunguliwa kesi, akishtakiwa kwa kosa la kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka.

Akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari waliotaka kujua upelelezi wa kesi hiyo umefikia wapi, licha ya kukamatwa kwa mtuhumiwa wa kesi hiyo, ambaye anaendelea kusota gerezani, IGP Mwema alisema upelelezi wa kesi unategemea kupatikana mapema kwa ushahidi husika, vinginevyo kesi za aina hiyo zinaweza kuchukua muda mrefu.

Hata hivyo, suala la mtu kufunguliwa kesi huku akiendelea kusota rumande, limezua sintofahamu ya aina yake, huku watu wakihoji upelelezi wa polisi kuchukua muda mrefu bila kukamilika, kwamba ni kumnyima haki mshtakiwa.

Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Thomas Mihayo alipotakiwa kuzungumzia hali hiyo, alisema dhamana ni haki ya mshtakiwa hivyo si vema mtu kunyimwa dhamana bila sababu.

Hata hivyo, alisema si kila kosa linaweza kuwa na dhamana na kwamba, hilo linategemea aina ya kosa husika.

“Makosa yanayozuia kuwa na dhamana ni yale ya jinai, lakini katika nchi zilizoendelea hata kama ni jinai lazima kwanza upelelezi ufanyike kabla ya kumkamata mtuhumiwa, vinginevyo ni kinyume cha utaratibu.

“Hapa kuna mambo mawili yanaweza kufanyika, upelelezi lazima kwanza ukamilike ndipo akamatwe mtuhumiwa, lakini pia wanaweza kumkamata mtuhumiwa, halafu akaachiwa kwa dhamana na upelelezi ukaendelea kufanyika ingawa hapa kwetu yote hayafanyiki,” alisema Jaji Mihayo.

Kuhusu suala la Ulimboka, alisema mtuhumiwa huyo raia wa Kenya, ameendelea kusota rumande kwa sababu ya kukosa wanasheria wa kumsimamia na kuhakikisha haki inatendeka.

Alisema kama Mlundi, angekuwa na wanasheria wangemsaidia kuonyesha ile kesi si halisia.

Alisema wakati mwingine kile kinachoitwa mada huwa hakipo, kwa lugha ya kisheria zinaitwa ‘murder toy’, hivyo kesi za aina hiyo wanasheria huzikatia rufaa kutokana na mazingira yaliyopo.

Mbali na hoja hizo za kisheria, kwa nyakati tofauti, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova aliwahi kusema suala la Ulimboka limefungwa na limebaki mikononi mwa uongozi wa juu wa jeshi hilo.

Pia Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso alisema suala la Dk. Ulimboka, limefungwa kwa sababu tayari liko mahakamani.

Sakata hilo la Dk. Ulimboka liliendelea kuwa mwiba mkali, baada ya baadhi ya vyombo vya habari pamoja na Ulimboka mwenyewe kumtaja mtu mmoja, Rama Ighondu mmoja wa wafanyakazi wa Ikulu kuwa ndiye alihusika kumteka.http://www.mtanzania.co.tz
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top