Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

JK asisitiza kuendelea kukopa

 

 Rais Jakaya Kikwete amesema Serikali itaendelea kukopa kwa ajili ya maendeleo, kwani haiwezi kuendesha taifa kwa kutegemea kodi pekee.
Akiwa kwenye ziara ya Mkoa wa Dar es Salaam jana, Rais Kikwete alitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo, ikiwamo uzinduzi wa maabara ya kisasa ya Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) na Chuo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano Veta Kipawa
Alisema mikopo inalipwa kwa kipindi kirefu na riba yake ni nafuu na kwamba, anashangazwa na wanasiasa ambao alidai wengi ni wasomi ambao wamekuwa wakidanganya watu na kuwatia hofu.

“Kumekuwa na siasa nyingi kwamba tunadaiwa na kila Mtanzania anatakiwa alipe Sh400,000, mnadhani tunakopa na kulipa kesho?” alihoji Rais Kikwete.
Akitoa mfano, alisema daraja la Malagarasi limejengwa kwa mkopo na kwamba, riba yake ni asilimia 0.02 na utalipwa kwa miaka 40.

“Hatuachi kukopa ng’o, ukiacha wengine kama Kenya watakwenda watachukua na kupata maendeleo halafu wewe unabaki hapohapo ulipo,” alisema.

Katika hatua nyingine, Rais Kikwete amewaagiza watendaji wa Dar es Salaam kujenga hospitali maalumu za uzazi na watoto, lengo likiwa ni kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Alisema haiwezekani kila mara kutoa taarifa bila kuwapo kwa suluhisho la matatizo yanayotolewa ufafanuzi.
Rais Kikwete alisema katika kuboresha sekta ya afya na upatikanaji wa huduma, lazima kuhakikisha zinajengwa hospitali maalumu za uzazi na watoto ili kupunguza msongamano uliopo hivi sasa.
“Huwa najiuliza ninyi madiwani mnapokutana katika vikao vyenu mnazungumza kitu gani, kugawa viwanja?” alihoji Rais Kikwete huku watendaji mbalimbali wakiangua vicheko.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top