KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) itadhamini bonanza la vyombo mbalimbali vya
habari litakalofanyika Aprili 6 mwaka huu viwanja vya Leaders Klabu, Dar
es Salaam likiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo
Tanzania (TASWA).
Akizungumza katika mkutano
na wanahabari kutambulisha bonanza hilo Dar es Salaam jana, Ofisa
Uhusiano wa TBL, Doris Malulu alisema huu ni mwaka wa tano mfululizo kwa
kampuni yake kudhamini bonanza linaloandaliwa na TASWA na kwamba
wamekuwa na matumaini makubwa na chama hicho ndiyo sababu wanakubali
kushirikiana nacho kila mwaka.
Malulu
alisema zaidi ya Sh. Milioni 50 zitatumika kwa ajili ya bonanza hilo na
kusisitiza kuwa lengo la kampuni yake ni kuona linakuwa na mafanikio
makubwa kuliko mengine yaliyopita.
“Wanahabari
ni wadau wetu wakubwa, hivyo kupitia TASWA tunaona ni njia nzuri ya
kutuunganisha na kukaa pamoja kutafakari masuala mbalimbali,” alisema
Malulu.
Kwa
upande wake Katibu Mkuu wa TASWA, Amir Mhando aliishukuru TBL kwa
udhamini huo na kusema kuwa zaidi wa washiriki 1,500 wanatarajiwa
kuhudhuria tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA kila mwaka likijulikana
kama Media Day Bonanza.
“Lengo
la bonanza letu ni kuwaweka pamoja waandishi wote wa habari bila kujali
ni wa siasa, michezo, uchumi, afya na mambo mengine pamoja na
wafanyakazi wa vyombo mbalimbali vya habari, ili kubadilishana mawazo na
kufurahi pamoja,” alisema.
Alieleza
kuwa bonanza hilo litaambatana na michezo mbalimbali itakayohusisha
vyombo vyote vitakavyoshiriki na pia kutakuwa na burudani ya muziki
kutoka katika moja ya bendi kubwa za muziki wa dansi hapa nchini, ambayo
itatangazwa siku zijazo.
Bonanza
la mwaka jana lilifanyika ukumbi wa Msasani Beach Klabu, ambapo mgeni
rasmi alikuwa Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ambaye pia ni
Mbunge wa Urambo Mashariki na aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, Samuel
Sitta.
Pamoja
na mambo mengine, Sitta alikabidhi zawadi za vikombe na medali kwa
washindi mbalimbali walioibuka siku hiyo, pia alipata fursa ya
kuzungumza na washiriki zaidi ya 1,500 wa bonanza hilo
.na fullshangwe
Post a Comment