* Achangisha mil. 200/-
WAZIRI Mkuu aliyejiuzulu, Mhe. Edward
Lowassa alichangisha zaidi ya sh milioni 200 fedha taslimu na ahadi katika
harambee ya uje
nzi wa chuo cha afya
wilayani hapa, kiongozi huyo amesifiwa kwa uthubutu wa kuagiza na
kutenda.
Sifa hizo zilitolewa na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Karatu na Diwani wa Kata ya Ganako, Lazaro Maasai
(CHADEMA) wakati wa harambee ya chuo hicho kinachomilikiwa na Kanisa la Kiinjili
la Kilutheri Tanzania (KKKT) Karatu kwa ushirikiano na
serikali.
“Wewe ni Waziri Mkuu
pekee uliyekuwa unathubutu na kutekeleza kwa vitendo,” alisema Maasai huku
akikumbushia jinsi alivyosimamia ujenzi wa shule za sekondari za kata
nchini.
Alisema ile ndoto yake
ya kuwaendeleza Watanzania kielimu, Karatu waliifanyia kazi na ndiyo maana
wanajenga chuo hicho cha afya ili wale watoto wanaomaliza kidato cha nne waweze
kuendelea na masomo.
Askofu wa Dayosisi ya
Kaskazini Dk. Martine Shao, akizungumza katika ibada hiyo alimshukuru Mungu kwa
kujibu maombi yao.
Alisema siku zote kanisa
huwa halibahatishi, na kwamba anaamini Mungu amempa Lowassa vipaji
mbalimbali.
“Mungu amekubariki na
ndiyo maana ukitoa kauli nchi nzima inafuata na kote ulikofanya kazi tumeona
kazi yako, Watanzania wanamshukuru Mungu.
“Siku zote mtu mwenye
vipaji ana ndoto nyingi, umesimamia ndoto zako vizuri, hatujui huko mbele
tuendako, tunamuomba Mungu akulinde na kukubariki katika wajibu wako,”
alisema.
Lowassa akizungumza
kabla ya kuanza kuchangisha, aliwaeleza waumini hao kwamba zipo sababu kadhaa
ambazo zimekuwa zikimsukuma kutumika katika harambee.
Tanzania
Daima
Post a Comment