Makamu wa Kwanza wa Rais wa
Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad amezindua vilabu 15 vya uchangiaji damu
salama kisiwani Pemba kwa azma ya kuwahamasisha wananchi kisiwani humo
kujitokeza kwa wingi kuchangia damu, ili iweze kuwasaidia wagonjwa wanaohitaji
kupatiwa huduma hiyo.
Uzinduzi wa vilabu hivyo
ambao uliambatana na Tamasha la Michezo, ulifanyika leo 17/3/2013 katika viwanja
vya Ole Kianga, mkoa wa Kaskazini Pemba.
Akizungumza katika hafla
hiyo, Makamu wa Kwanza wa Rais aliwataka wananchi wasipuuze tabia kuchangia damu
kwa sababu ni kuokoa maisha ya binaadamu na kila mtu anaweza kupata na shida
ambayo itamfanya ahitaji kuchangiwa damu.
“Utaratibu wa kuchangia
damu ni jambo zuri la kuokoa maisha ya watu, wananchi jitokezeni kwa wingi
kuchangia benki ya damu na wala msiogope kwenda kutolewa damu”alihimiza Maalim
Seif.
Aliwahimiza wafanyakazi wa
serikali, wakiwemo askari wa vikosi mbali mbali vya ulinzi na usalama kujitokeza
kwa wingi na kuendeleza utaratibu wa kuchangia damu
salama.
Alieleza kuwa ili benki ya
damu Zanzibar iweze kuwa na akiba ya kutosha na pale yanapotokea mahitaji, kama
vile ajali na wakonjwa wanaohitaji kuipata bila ya taabu, wananchi wote sifa za
kuchangia damu wajitokeze kwenda kuchangia.
Akizungumza
katika hafla hiyo, Katibu wa Jumuiya ya Uchangiaji damu kwa hiari Zanizbar, Dk.
Mussa Magarawa alisema mwamko ulioanza kuoneshwa na baadhi ya wananchi Zanzibar
kwa kujitokeza kuchangia damu umeweza kusaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza uhaba
wa damu na kuokoa vifo vingi vya akinamama wajawazito na watoto
wadogo.
Dk. Magarawa
allisema hivi sasa Zanzibar kuna wachangiaji damu wa uhakika 8,500 ambapo wengi
wao wapo kisiwani Unguja na kuna vilabu vipatavyo 75 vya wachangiaji
damu.
Hata hivyo
alisema msukumo mkubwa unahitajika kisiwani Pemba ambapo bado mwamko wa wananchi
kujitokeza kuchangia damu ni mdogo zaidi.
Afisa Mdhamini
Wizara ya Afya, Pemba, Dk. Ukasha Daudi Ukasha alisema Wizara hiyo inachukua
juhudi kubwa kuhakikisha hospitali kuu kisiwani humo zinakuwa na sehemu za
kuhifadhia damu na kuhakikisha huduma ya damu inakuwepo ya kutosha wakati
wote.
Alisema ipo haja viongozi
waunge mkono vilabu vya kuchangia damu salama na wao wenyewe wajiunge na wawe
wanachama, hatua ambayo itawafanya wananchi wengi zaidi kuhamasika na
kujiunga

Post a Comment