Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL, AMALIZA ZIARA YAKE MKOA WA MARA AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA ZA WATUMISHI WA UMMA MUSOMA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa, wakifurahia kwa pamoja baada Makamu kuweka Jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Nyumba za Watumishi wa Umma, wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana Machi 5, 2013 Wilaya ya Musoma, Mkoa wa Mara, wakati Makamu akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani humo. Picha na OMR
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal, wakisikiliza maelezo na kuoneshwa Ramani za ujenzi wa nyumba za watumishi wa Umma, wakati Makamu alipofika eneo hilo kuweka jiwe la msingi Ujenzi wa nyumba hizo jana Machi 5, 2013. Picha na OMR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, mkewe Mama Asha Bilal, Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, Mkuu wa Mkoa wa Mara, Gabriel Tupa na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa TBA, mara baada ya Makamu kuweka jiwe la Msingi katika mradi wa ujenzi wa Nyumba za watumishi wa Umma, jana Machi 5,2013. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AZUNGUMZA NA WANACHAMA WA CCM MUSOMA MJINI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati alipokutana na Wanachama wa CCM mkoa wa Mara katika Ukumbi wa CCM mkoa uliopo eneo la Nyasho Musoma mjini, wakati Makamu akiwa katika ziara yake ya siku mbili mkoani Mara. Picha na OMR

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWAHUTUBIA WANANCHI WA MUSOMA MKOA WA MARA
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwahutubia wananchi wa Musoma Mjini Mkoa wa Mara, katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Uwanja wa Mukendo jana Machi 5, 2013 ikiwa ni siku ya mwisho ya zaiara yake mkoani Mara. Picha na OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wazee wa mkoa wa Mara wakati akiagana nao baada ya kuwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo jana Machi 5, 2013.ikiwa ni siku ya mwisho ya zaiara yake mkoani Mara. Picha na OMR
Juu na chini ni Waziri wa Ujenzi, Dkt. John Pombe Magufuli, akizicharaza Tumba za bendi ya Msondo Ngoma, wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani Mara jana Machi 5, 2013, wakati Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mkoa huo. Kushoto ni wanamuziki wa bendi hiyo, wakimshabikia. Picha na OMR
Wanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, wakionyesha umahiri wao wa kupuliza 'midomo ya bata' wakati wa bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Mukendo Musoma mjini Mkoani Mara jana Machi 5, 2013, wakati Makamu wa Rais Dkt. Bilal, alipokuwa akiwahutubia wananchi wa mkoa huo. Picha na OMR

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top