Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Jengo la Ghorofa
16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki.
Makamu amefika kushuhudia Shughuli za uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi
sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa kuwa imefikia watatu na waliookolewa
wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman
Kova.
Uokoaji
ukiendelea.....
Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiondoka eneo la tukio
baada ya kuangalia Jengo la Ghorofa 16, lililoporomoka lenyewe leo asubuhi
katika Mtaa wa Indra Ghand na Zanaki. Makamu amefika kushuhudia Shughuli za
uokoaji ambazo zinaendelea, ambapo hadi sasa idadi ya watu waliofariki imeelezwa
kuwa imefikia watatu na waliookolewa wakiwa hai ni 17, kwa mujibu wa Kamanda wa
Polisi wa Kanda Maalum, Suleiman Kova.
Askari Jeshi wakikokota
Jenereta kubwa kusogeza eneo la tukio ili kuhakikisha mwanga unapatikana
kurahisisha shughuli za uokoaji hadi usiku, baada ya giza
kuingia.
Post a Comment