![]() |
Edward Lowassa |
Na Mwandishi Wetu, Arusha
WAZIRI Mkuu Mstaafu Edward Lowassa, anatarajiwa kuwa
mgeni Rasmi katika mbio za Sokoine Marathon, zinatakazofanyika, Aprili 12,
mwaka huu, wilayani Monduli, mkoani Arusha.
Mbio hizo zitafanyika katika kijiji
alichozaliwa na kuzikwa waziri mkuu Edward Moringe Sokoine ikiwa ni siku ambayo
taifa itaadhimisha kumbukumbu ya kifo cha kiongozi huyo mkuu katika historia ya
taifa la Tanzania.
Akithibitisha hilo Mratibu wa mbio za Sokoine Marathon 2013, Wilhelm Gidabuday alisema kuwa tayari wameshapata uthibitisha wa kuwepo kwa kiongozi huyo akiongozana na viongozi wengine wakuu wa nchi wakiwemo Mawaziri na Wabunge. “Kutokana na wadhifa na heshima aliyokuwa nayo Marehemu Sokoine tumeona ni vizuri kuwaalika viongozi wetu wakuu wa nchi,n watu wengi tu watakuwepo, wabunge, mawaziri wakiongozwa na mheshimiwa Lowassa, wananchi wa kada mbalimbali, lengo ni kumpa heshima inayostahili kingozi wetu,” alisema Gidabuday. Kwa upande wake mjumbe wa kamati ya maandalizi aliyepewa jukumu la kuwasiliana na viongozi ikiwa ni pamoja na Mgeni Rasmi, Mbunge wa viti maalum jimbo la monduli (CCM), Namelok Sokoine alisema kuwa, tayari wameshapata uhakika wa uwepo wa Lowassa katika mbio hizo. |
![]() |
Sokoine |
likuwa tunatarajia kumpata kiongozi wetu wa nchi Mbio za
Sokoine Marathon ambazo ni za kwanza kufanyika katika historia ya nchi hii
katika maadhimisho ya kumbkumbu ya kifo cha kiongozi wa ngazi za juu wa taifa
letu zinatarajiwa kushirikisha wakimbiaji zaidi ya 500 ambapo mpaka sasa tayari
wanariadha 300 wameshathibitisha kushiriki.
Akizungumzia swala la kutoa namba pamoja na usajili, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Arusha (ARAA), Joseph Jorwa alisema tayari utaratibu wa kuandaa namba umeshakamilika na kuongeza kuwa zoezi la usajili utafanyika baada ya sikuukuuu za Pasaka, katika Ofisi za ARAA, zilizoko katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa ada ya sh. 2000 za Tanzania.
Akizungumzia swala la kutoa namba pamoja na usajili, Mwenyekiti wa Chama cha Riadha Arusha (ARAA), Joseph Jorwa alisema tayari utaratibu wa kuandaa namba umeshakamilika na kuongeza kuwa zoezi la usajili utafanyika baada ya sikuukuuu za Pasaka, katika Ofisi za ARAA, zilizoko katika uwanja Sheikh Amri Abeid jijini Arusha kwa ada ya sh. 2000 za Tanzania.
Sokoine Marathon zitahusisha mbio za
kilometa 10 na kilometa 2 kutembea na kukimbia na zitatanguliwa na misa maalum
zitakazofanyika katika kanisa la katoliki alililokuwa ni muumini kijijini kwake
na zinatarajia kukutanisha watu mbalimbali kumuombea kiongzi huyo.
Post a Comment