Kupitia ukurasa wake wa facebook Mh. January Makamba ameandika yafuatyao mara baada ya kuongea na Ndugu Absalom Kibanda:
"Hivi punde, nimemaliza kuongea kwa simu na Ndugu Absalom Kibanda akiwa hospitalini Afrika Kusini. Yupo kwenye maumivu makali lakini kwa maana ya spirit, hajabadilika bado ni yule yule Kibanda mcheshi na mwenye bashasha. Hili limenitia moyo sana. Katika kuugua hili ni jambo muhimu hasa ukizingatia yaliyomkuta. Madaktari wameshaanza kumtibu. Tumuombee apone haraka. Pia tunatarajia kupata ukweli kamili na kwa haraka kuhusu mazingira ya tukio lililomkuta na wahusika wapatikane, wakamatwe na wapelekwe mbele ya vyombo vya sheria.
Kwenye picha hii hapa, yupo na dada yangu Mwamvita Makamba aliyeenda kumjulia hali na kutoa msaada wowote unaohitajika."
Post a Comment