|
Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria katika Wizara
ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Irene Kasyanju akizungumza
na Mkurugenzi wa Idara ya Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Denmark,
Balozi Thomas Winkler kuhusu ushirikiano kati ya Tanzania na Denmark katika
masuala ya sheria na mikataba mbalimbali ya kimataifa ikiwemo masuala ya
kupambana na Uharamia. Mazungumzo hayo yalifanyika Wizarani tarehe 20 Machi,
2013. |
|
Balozi Winkler akichangia hoja wakati wa
mazungumzo hayo huku Balozi Kasyanju
akimsikiliza. |
|
Balozi Kasyanju akimsikiliza Balozi Winkler
wakati wa mazungumzo yao. Wengine katika picha ni Bw. Elisha Suku (kulia), Afisa
Mambo ya Nje katika Kitengo cha Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje, Bi. Mille Sofie
Brandrup (kushoto), Afisa kutoka Idara ya Sheria za Kimataifa, Wizara ya Mambo
ya Nje ya Denmark na Bw. Lars Bo Kirketerp Lund, Afisa kutoka Ubalozi wa Denmark
hapa nchini. |
on Wednesday, March 20, 2013
Post a Comment