Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, wapili kutoka kushoto akikata utepe kuashiria kufunguliwa rasmi kwa Programu ya Mafunzo kazini kwa askari wote nchi nzima yaliyofanyika jijini Dar es salaam, akifuatiwa na Kamanda wa Kanda Maalumu ya Dar es salaam DCP Suleiman Kova, Mkuu wa chuo cha Taaluma ya Polisi (DPA) ACP Ally Lugendo na kushoto ni Mkuu Kitengo cha wa Mafunzo SACP Alice Mapunda.( Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Said Mwema, akiwa na maofisa wa Polisi wakifuatilia kwa karibu uzinduzi wa program ya mafunzo kazini kwa kutumia mtandao, tukio hilo lilifanyika jijini Dar es salaam.( Picha na Frank Geofray wa Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema akikagua program ya Mafunzo kazini kwa wakaguzi wa Polisi pamoja na askari, ukaguzi huo ulifanyika Makao makuu ya Polisi jiji Dar es salaam. Picha na Frank Geofray- Jeshi la Polisi)
Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Said Mwema akikagua Utekelezaji wa Programu ya mafunzo kazini kwa maofisa wa Polisi( kushoto ni Msemaji wa Jeshi la Polisi Advera Senso), ukaguzi huo ulifanyika Makao Makuu ya Jeshi Polisi ( picha na Frank Geofray- Jeshi la Polisi) .
Post a Comment