Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala Jerry Silaa akiwasili katika Shule ya Msingi Kigilagila iliyopo maeneo
ya Gongo la Mboto kama mgeni rasmi katika hafla fupi iliyoandiliwa na mfuko wa
Pensheni wa PPF ya kukabidhi vitabu kwa wanafunzi wa shule
hiyo.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya
wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akitambulishwa kwa Meneja wa Penesheni Bi.
Chevu Sepeku( kushoto) mara baada ya kuwasili katika shule hiyo. Wa pili kushoto
ni Meneja wa Mfuko wa Pensheni Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba na Wa pili kulia
ni Afisa Uhusiano wa Pensheni wa PPF Bi. Lulu Mengele.
Mgeni rasmi Mstahiki Meya
Jerry Silaa akiteta jambo na mmoja wa wanakikundi cha kwaya cha shule hiyo mara
baada ya kuwasili.
Kwaya ya Shule ya Msingi
Kigilagila ikipiga wimbo wa Taifa kuashiria kuanza kwa hafla
hiyo.
Meza kuu wakiupa heshima
wimbo wa Taifa: Mgeni rasmi Mstahiki Meya Jerry Silaa (wa pili kushoto), Meneja
wa Penesheni Bi. Chevu Sepeku( kulia) , Wa pili kulia ni Meneja wa Mfuko wa
Pensheni Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba na kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Kigilagila Verian Mfugale.
Mwalimu Mkuu wa Shule ya
Msingi Kigilagila Verian Mfugale akiukaribisha ugeni katika shule hiyo wakati wa
hafla fupi ya kukabidhi zawadi za vitabu shuleni hapo pamoja na kwa watoto
wawili yatima ambao wazazi wao walikuwa ni wanachama wa mfuko wa Pensheni wa PPF
na kuendelea kusomeshwa kupitia FAO LA ELIMU linatolewa na mfuko wa Penesheni
wa PFF.
Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala Jerry Silaa akizungumza jambo na Meneja wa Mfuko wa Pensheni Kanda ya
Ilala Bw. Evans Musiba wakati wa hafla fupi ya kukabidhi vitabu iliyoenda
sambamba na Kampeni ya Kutangaza FAO LA ELIMU.
Mstahiki Meya wa Manispaa
ya Ilala Mh. Jerry Silaa akizungumza na walimu na wanafunzi wa shule ya
Kigilagila na kufafanua kuwa mambo yanayofanywa na Mfuko waPensheni wa PPF
katika kurekebisha baadhi ya mafao yake haswa fao la kifo, si tu yatasaidia
kuwapa elimu wanafunzi wanaoguswa bali yatatia mkono katika kuboresha elimu
katika mfumo mzima wa taifa letu na moja kwa moja katika maendeleo ya uchumi wa
nchi yetu.
Aidha Mh. Silaa ametoa wito
kwa watanzania akisema kwa kuwa sasa mifuko hii ya pensheni imefungua milango,
sio kwa watu walioajiriwa pekee ndio wanaopaswa kujiunga na mifuko hii ya
pensheni, lakini hata kwa watu waliojiajiri, wakulima na hata wafugaji wana
uwezo kabisa kisheria kujiunga na mifuko ya pensheni na kunufaika
nayo.
Pia ameupongeza mfuko wa
PPF kwa yale wanayoyafanya kwa watoto wa watu waliofariki wakiwa wanachama wa
mfuko huo, ambapo takwimu zinaonyesha kuwa kwa mwaka 2012 jumla ya wanafunzi 1,
333 wamelipiwa gharama mbalimbali zilizofikia jumla ya shilingi milioni 682.9
kitu ambacho ni jambo la kupigiwa mfano.
Meneja wa Mfuko wa
Pensheni wa PPF Kanda ya Ilala Bw. Evans Musiba akielezea nia ya kutembelea
shule hiyo ni kutoa msaada wa vitabu kwa sababu tunaamini kwamba vitabu
tutakavyo vitoa vitawasaidia wanafunzi waliopo hapa kuweza kupata elimu nzuri na
kufanya vizuri katika mitihani yao na vilevile hawa ndio viongozi wa baadae.
Vilevile katika hii shule ya Kigilagila sisi kama PPF tuna wanafunzi ambao
tunawasomesha hivyo sisi ni wadau wa shule hii na tunatumia fursa hii kuwashauri
waalimu na pia wazazi kujiunga na mfuko huu kwa manufaa ya
baadae.
Meneja wa Penesheni PPF
Bi. Chevu Sepeku akitoa elimu kwa wageni na wanafunzi waliohudhuria hafla hiyo
kuhusiana na taratibu za utoaji wa mafao ya Elimu na kufafanua kuwa hutolewa ili
kugharamia sehemu au gharama zote zinazohitajika katika elimu ya mtoto wa
mwanachama aliyefariki ambapo gharama hizo ni kuanzia elimu ya chekechea hadi
kidato cha nne.
Mstahiki Meya Jerry Silaa
akikabidhi zawadi kwa mtoto wa darasa la Saba Ummy Abdalah kwa niaba ya
wanafunzi wenzake. Ummy Abdalah ni miongoni mwa wanafunzi wanaosomeshwa na PPF
kutumia FAO LA ELIMU baada ya wazazi waliokuwa wananchama wa mfuko huu kufariki
dunia.
Mtoto Shakila Abdalah wa
darasa la pili naye akipokea zawadi kutoka kwa Mstahiki Meya Jerry Silaa.
Kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Veriana Mfugale akishihudia tukio
hilo.
Wanafunzi wa shule hiyo
wakifanya mchezo wa kuigiza unaohamasisha wazazi kujiunga na Mfuko wa Pensheni
wa PPF kwa manufaa ya watoto wao hapo baadae hasa kwa suala la elimu kama
itatokea mzazi huyo kufariki.
Sehemu ya zawadi
zilizotolewa na mfuko wa Pensheni wa PPF wa Fao la Elimu kwa wanafunzi wa shule
ya msingi Kigilagila.
Mstahiki Meya Jerry Silaa
akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo na kuwasisitiza kutilia mkazo
elimu wakati akigawa vitabu vya masomo mbalimbali kwa wanafunzi wa shule
hiyo.
Post a Comment