Kalonzo Musyoka. |
MGOMBEA mwenza wa waziri mkuu wa Kenya
Raila Odinga, amesema kuwa kuna ushahidi kuonyesha kuwa kuna hujuma dhidi yao
katika dhughuli ya kuhesabu kura inayoendelea katika ukumbi wa Bomas, na kwamba
shughuli hiyo inastahili kusitishwa.
Hata
hivyo alisema kuwa haina maana kuwa wanaitisha maandamano.
Shughuli
ya kuhesabu kura ingali inaendelea ingawa kwa mwendo wa kinyonga baada ya tume
hiyo kutupilia mbali mitambo yake ya kuhesabu kura baada ya kugoma. Uhuru
Kenyatta angali anaongoza kwa idadi ya kura za wagombea wa urais akiwa na kura
2,660,379 dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga aliye na kura 1,996,181 lakini
matokeo rasmi yatajulikana tu mwishoni mwa juma.
Taharuki imetanda na kuna hali ya wasiwasi kwani tume ya uchaguzi
haijatangaza matokeo ya urais zaidi ya masaa arobaini na nane tangu wakenya
kupiga kura. Muungano wa CORD umesema kuwa unatafakari hatua za kuchukua baada
ya kudai hujuma katika shughuli inayoendelea ya kuhesabu kura za
urais.
Shughuli hiyo imekumbwa na utata hasa baada ya mitambo ya kuhesabu
kura ya tume ya uchaguzi kukumbwa na hitilafu. Hatua hii imelazimu tume hiyo
kuanza kuhesabu kura upya katika kitovu cha kupokea matokeo ya kura za urais
kwenye ukumbi wa Bomas viungani wa mji wa Nairobi.
Kalonzo
Musyoka ambaye ni mgombea mwenza wa Raila Odinga, amehutubia waandishi wa habari
mjini Nairobi na kusema kuwa muungano wa CORD, unataka shughuli hiyo ya kuhesabu
kura za urais kusitishwa mara moja na kuanzishwa upya wakitumia stakabadhi
kutoka kwa makarani wa kura jambao ambalo linafanywa kwa
sasa
Musyoka
vile vile amesema kuwa muungano huo una tashwishi kuhusu baadhi ya matokeo
wakisema sio ya kweli kwa kuwa hayawiani na yale waliyoyaleta maajenti wao.
Aliendelea kwa kusema kuwa baadhi ya matokeo yako juu kuliko idadi ya wapiga
kura katika baadhi ya maeneo ambako kura zilipigwa.
Musyoka
amesisitiza kuwa tatizo hilo limetokana na kugoma kwa mitambo ya kupiga kura na
pia kuanza upya kwa shughuli ya kuhesabu kura kwa kutumia mfumo wa
zamani.
Musyoka
alisema kuwa tume ya uchaguzi inastahili kutumia mitambo ya elektroniki kuhesabu
kura kama inavyoagiza katiba ya nnchi, huku akiongeza kuwa muungano huo ungali
unatafakari hatua za kuchukua ingawa kwa kufuata sheria. Moja ya hatua
inazotafakari kuchukua ni kwenda mahakamani kuitaka mahakama kusimamisha
shughuli ya kuhesabu kura na kuanza tena.
Post a Comment