Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akizindua kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi katika hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam.Mwanasiasa mkongwe Mzee Kingunge Ngombale Mwiru akisisitiza jambo wakati uzinduzi wa kitabu historia ya Hayati Sheikh Kaluta Amri Abedi katika hafla iliyofanyika leo kwenye ukumbi wa Karimjee jijini Dares Salaam.Kushoto ni Balozi Mstaafu Job Lusinde na kulia ni Brigedia Hashimu Mbita.
…………………………………………………………….
MWANASIASA mkongwe nchini
Kingunge Ngomble Mwilu amewataka Watanzani kuienzi Lugha ya Kiswahili kama
nyenzo itakayosaidia katika kukuza na kuleta maendeleo katika elimu
nchini.
Kingunge aliyasema hayo
jijini Dar es Salaam jana, wakati wa uzinduzi wa kitabu cha Historia ya Hayati
Sheikh Kaluta Amri Abed, kilichoandikwa na Mathias Eugen ambapo uzinduzi huo
uliandaliwa na familia ya Kaluta na baadhi ya wataalamu wa lugha hiyo kutoka
Bakita.
Alisema anathamini uzinduzi
wa kitabu hicho ambacho kimekusanya kazi mbalimbali zilizofanywa na Hayati
Kaluta wakati wa uhai wake.
Kingunge alisema kila Taifa
duniani ili liweze kupiga hatua mbalimbali za maendeleo ni lazima liwe na lugha
inayofahamika vizuri na raia wake ambapo kwa Tanzania rugha rasmi ni
Kiswahili.
“Lugha ni chombo cha msingi
kwa binadamu pia inatofautisha kati ya binadamu na viumbe vingine ambapo kupitia
lugha ndipo tunapokuza uwezo wa kufikiri kwani huwezi kukuza uwezo wa kufikiri
biala ya kuwa na lugha ya kueleweka”alisema Kingunge.
Aidha, aliwapongeza akina
Hayati Kaluta na wenzake kwa kuiheshimu lugha hiyo ambayo mara zote imekuwa
ikitumika katika kujenga umoja wa taifa hilo.
Aliwasa Watanzani kuacha
tabia ya kukifanya Kiswahili kuwa ni tatizo na baadala yake kuwandaliwe mikakati
ya lugha hiyo ili iwe ya kufundishia katika vyuo vikuu nchi lengo likiwa kujenga
uelewa mzuli wa lugha, inayozungumzwa hata kwenye Umoja wa Mataifa
(UN).
Miongoni
mwa watu maarufu waliohudhuria katika uzinduzi huo ni pamoja na Balozi Job
Lusinde, Suleiman Hega, Hashim Mbita na wengine ambapo wote, kila mmoja
alisistiza matumizi ya lugha hiyo kwa
ufasaha.
Post a Comment