Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

"NJIANI KWENDA KWA RAIS" - 2


1 49656
Ndugu zangu,
Niliandika juzi, kuwa mwaka 1964 yawezekana kabisa ndio ulikuwa ni mwaka mgumu sana kwa Julius Nyerere katika kipindi chake chote cha Uongozi wa nchi hii.Ni mwaka uliokuwa na matukio makubwa yaliyoitikisa nchi na Rais mwenyewe. Kulikuwa na Mapinduzi ya Zanzibar ya Januari 12. Kukawa pia na uasi wa jeshi wa Januari 20, na matukio mengine yakafuatia.

Mwandishi Stig Holmqvist kwenye kitabu chake; Pa vag till presidenten – ‘ Njiani kwenda kwa Rais’, anaulezea mkutano mgumu kati ya Julius Nyerere na Balozi wa Marekani Tanzania, Leonhart.Julius Nyerere alikwenda mwenyewe kwa Balozi kufafanua kilichotokea na kupelekea kuridhia Balozi mdogo wa Marekani Unguja afukuzwe nchini.
Ujumbe wa siri kwa njia ya telegramu kutoka kwa Balozi Leonhart kwenda White House na CIA unabainisha jambo hilo.Inaelezwa na Balozi huyo, kuwa siku hiyo ya mkutano wake na Julius, Januari 16, 1964, kuwa hali haikuwa nzuri.

Balozi Leonhart anasema; “ ....Nyerere alitingisha kichwa na hakutaka hata kuniangalia....”Tumeona, kuwa katika mkutano ule, Julius Nyerere, pamoja na kutambua mapungufu, lakini alikataa katakata kubadili msimamo wake wa kumfukuza balozi huyo mdogo wa Marekani.Julius alikuwa na miaka mitatu tu kama Rais. Alikuwa kijana wa miaka 42 tu. Na Chama chake cha TANU kilikuwa hakijatimiza hata miaka kumi. Na yeye mwenyewe, Julius, kumbukumbu za kutumia chaki za ubaoni kama mwalimu wa pale Pugu Sekondari huenda zilikuwa bado hazijamtoka. Lakini, pale kwa Balozi wa Marekani, alikaa na kuongea kama Rais wa Tanzania. Ndio, alikuwa Rais mchanga kwenye nchi changa. Julius hakuwa na uzoefu wa siasa za kimataifa na hasa inapohusu ‘ michezo ya wakubwa’- Marekani na Uingereza kwenye upande mmoja, na Soviet Union, China na Cuba kwenye upande wa pili.
Yawezekana pale Ubalozini Julius alikumbuka usemi wa wahenga; “ Kua uyaone!”Ikumbukwe, Julius alimfanya rafiki yake wa karibu, Oscar Kambona kuwa Waziri wa Ulinzi na Mambo ya Nje. Na Oscar naye hakuwa na uzoefu. Hivyo, wote wawili; Julius na Oscar.Miezi michache tu baada ya tukio lile Ubalozini, marafiki wawili; Julius na Oscar walifunga safari ya kwenda China. Ilikuwa ni mara yao ya kwanza kwa wote wawili kwenda China.Huko China Julius na Oscar waliiona China kwa ‘ miwani tofauti’. Ni nini kilitokea kwa marafiki wawili hawa, Oscar na Julius, waliporudi nyumbani?
Panapo majaliwa nitawasimulia...
Pasaka Njema.
Maggid,
Dar es Salaam
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top