Kamanda wa Polisi Mkoani
Dodoma David A. Misime-ACP
Na John Banda,
Dodoma
POLISI Mkoani Dodoma
inawashikilia watu watatu baada ya kuwakuta wakiwa na nyaya za Transfoma za
jumla ya 20 milion mali ya Tanesco.
Nyaya hizo aina ya kopa
zenye uzito wa kilo 76 na nusu zilikutwa kwa watu hao baada ya msako wa polisi
wakishirikiana na Shirika la umeme Tanzania Tanesco
Kamanda wa polisi mkoa
wa Dodoma David Misime alisema nyaya hizo za matumizi ya Transfoma hutumika kwa
kufanyia Winding na nyingine ni kwa ajili ya kuzuia Radi [earthing] na kwamba
imebainika ziliibiwa maeneo ya kizota na Ihumwa baada ya transfoma zake
kuangushwa.
Misime aliwataja
waliokamatwa kuwa ni Abdul Bakari 17 mkazi wa Chang'ombe, Stanel Shayo 26 muuza
vyuma chakavu Nkuhungu na Peter Kessy 50 mkazi wa Area E manispaa ya
Dodoma.
Aliongeza kuwa jeshi
hilo linamsaka Jamal Said Sondo wa Chang'mbe Juu aliyekimbia ya mfanyakazi wake
Abdul Bakari kukamatwa
Kamanda huyo amewataka
wote wanaojihusisha na biashara ya vyuma chakavu wajiepushe na kununua nyaya na
vifaa vingine vya Tanesco pamaja na vyuma vyote viavyohusiana na miundo
mbinu.
Wakati huohuo Jeshi hilo
linamshikilia Denis Sadala 38 mkazi wa Mazase Wilayani Mpwapwa Kwa kumkuta
akimiliki Gobore bila kibali, huku likiendelea kumsaka Matagi Charles 33 mkazi
wa kijiji hicho aliyekimbia na kutelekza Gobore alilokuwa akimiliki kinyume na
Sheria.
Na John Banda, Dodoma

Post a Comment