Jeshi la Polisi mkoani
Arusha linawasaka wanawake wawili kufuatia kifo cha kutatanisha cha mjumbe wa
Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Taifa kupitia
Mkoa wa Arusha, Benson Peter Mollel (26).
Inadaiwa kuwa wanawake
hao walikuwa na Mollel kabla ya kufariki dunia ghafla juzi katika chumba cha
hoteli moja jijini hapa.
Tukio hilo lilitokea
mchana baada ya mwili wa merehemu kugunduliwa na wahudumu wa hotel hiyo
walipotaka kukifanyia usafi chumba alichokuwa amelala marehemu huyo
.
Kamanda wa Polisi Mkoa
wa Arusha, Liberatus Sabas, alisema jana kuwa marehemu alifika hoteli hapo,
Machi 2 mwaka huu jioni na kupanga katika chumba namba 208.
Alisema Polisi baada ya
kupata taarifa za tukio hilo, wanaendelea na msako kuwatafuta wanawake hao ambao
walikuwa na marehemu kabla ya kukutwa na mauti ya ghafla.
Alisema kuwa mmoja wa
wanawake hao alikwenda na marehemu hotelini hapo saa 7.00 usiku na mwingine
alikwenda hotelini hapo asubuhi saa 5.00 asubuhi.
Sabas alisema polisi
baada ya kufika hotelini hapo walimkuta marehemu na kuchukua mwili wake na
kuhifadhi hospitali ya Mkoa Mount Meru.
Post a Comment