Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi cheti cha kuhitimu mafunzo ya muda mfupi kwa viongozi mbunge wa viti maalum Ester Bulaya leo katika kambi ya RUVU JKT.Rais Kikwete amefunga rasmi mafunzi hayo leo yaliyofanyika kwa wiki tatu.(Picha na Freddy Maro)
Wabunge Halima Mdee na Ester Bulaya pamoja na wenzao wakila kiapo wakati wa kuhitimu mafunzo ya muda mfupi yaliyofanyika katika kambi ya jeshi la Kujenga Taifa Ruvu JKT huko kibaha Mkoani Pwani leo.
Mbunge wa Kigoma CHADEMA,
Zitto Kabwe pamoja na Wabunge wenzake kadhaa vijana leo wakemaliza rasmi mafunzo
yao ya awali ya JKT katika kambi ya Mgambo 835KJ kilichopo Mkoani
Tanga.
Pichani juu ni Zitto Kabwe
akijiandaa kwenda katika gwaride la mwisho na picha chini akiwa shambani pamoja
na Mbunge mwenzake Iddi Azan, Abdallah haji, Raya Ibrahim na Antony Mbassa
kambi ya Mgambo 835KJ.

Aidha Zitto Kabwe amesema
anafuraha iliyo pitiliza kumaliza mafunzo hayo na ameweka historia ya kubwa
katika maisha yake hii leo. Anapasha zaidi katika wakati wa Zoezi la kulenga
shabaha alifanikiwa kulenga risasi 3 akiwa amelala, 3 akiwa amepiga magoti na 1
akiwa amesimama. NA FATHER KIDEVU





Post a Comment