Spika wa Bunge la Tanzania Mhe. Anne Makinda (kulia) akimkaribisha Balozi wa Rwanda hapa nchini Tanzania, Mhe. Dkt. Ben Rugangazi, wakati Balozi huyo alipomtembelea Spika ofisini kwake Dar es Salaam leo. Katika mazungumzo yao, Balozi Rugangazi alimuomba Spika kupitia Bunge nchi mbili hizi zizidi kuimarisha mahusiano mzuri yaliyopo.
Spika Makinda alimhakikishia Balozi Rugangazi kulisimamia jambo hilo huku akimweleza kwa muhtasari nia ya mabadiliko ya Bunge ya kuanza mkutano wake wa Bajeti mwezi Aprili badala ya mwezi Juni kama ilivyozoeleka. Mkuu huyo wa mhimili wa Bunge amesema hatua hii itaisaidia serikali kuanza kutumia fedha za mapato na matumizi mara tu mwaka wa fedha wa serikali (Julai Mosi) unapoanza. “Siku ya kusomwa bajeti kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki itabakia kuwa ni ile ile ila sisi tutaanza kujadili wizara zote za kisekta isipokuwa wizara ya Fedha hadi mwezi Juni,” alisema Spika na kuongeza.
Balozi Rugangazi aliifurahia hatua hiyo huku akisisitiza kuwa Rwanda inayo mengi ya kujifunza kutoka Tanzania. Aidha Balozi huyo alitoa mwaliko na taarifa ya maadhisho ya siku ya ‘Utu wa Binadamu’ ambayo taifa la Rwanda huadhimisha kila tarehe 7 Aprili kwa ajili kuwakumbuka wale wote waliouawa katika mauaji ya kimbari ya mwaka 1994 ambapo watu takriban milioni moja waliuawa kikatili kufuatia mchafuko baina ya kabila la Wahutu na Watutsi.
Na Prosper Minja – Bunge
Post a Comment