Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Shilingi bilioni 18 kutumika katika uchimbaji wa visima



Na Frank John-Maelezo
pic3Jumla ya shilingi bilioni 18 zitatumika kwa ajili ya uchimbaji wa visima 20 vya maji vitakavyokuwa na uwezo wa kuzalisha zaidi ya lita milioni 266 kwa siku katika maeneo ya Kimbiji wilaya ya Temeke na Mpera wilayani Mkuranga kuanza mwezi wa sita mwaka huu na kukamilika mwezi wa sita mwaka 2014.
Hayo yamesemwa jana na afisa mtendaji mkuu wa mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA)
wakati akiwasilisha ripoti ya utendaji kwa kamati ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji ilipotembelea maeneo ya miradi ya visima hivyo.
Mutalemwa alisema kwamba utafiti uliofanywa umeonesha kuwa maji hayo ni safi na salama kwa matumizi ya binadamu na tayari mkandarasi kwa ajili ya kutekeleza wa mradi huo ameshapatikana . Pia mpango huo utahusisha maeneo kadhaa ikiwemo upanuzi wa kituo cha Ruvu juu ambao utaanza Julai mwaka huu na kukamilika Machi mwaka 2015.
“Tumeandaa mpango maalum wa kuhakikisha tunatatua tatizo la maji safi linalowakabili wakazi wa jiji la Dar es Salaam ikiwa ni pamoja na kujenga bwawa la Kidunda kuanzia Septemba mwaka huu na upanuzi wa mtandao wa mabomba utakaoanza mwakani na miradi yote hii itakamilika mwaka 2015”, alisema Mutalemwa.
Aliitaja miradi mingine katika mpango huo kuwa ni upanuzi wa mfumo wa majitaka unaotarajiwa kuanza mwakani na kukamilika mwaka 2016 na upanuzi wa mtambo wa Ruvu Chini.
Kwa upande wa mradi wa upanuzi wa Ruvu Chini ambao unagharamiwa na Serikali ya Marekani kwa gharama ya zaidi ya shilingi Bilioni 57, Mutalewa alisema kuwa utaongeza uwezo wa upatikanaji wa maji lita milioni 270 kwa siku.
Naye Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Dk. Binilith Mahenge alisema kuwa shilingi bilioni 27 zimetengwa kwa ajili ya kulipa fidia kwa wananchi watakaotakiwa kupisha mradi huo na aliwataka wananachi wa jiji la Dar es Salaam kuipa Serikali muda wa kufanya kazi hasa za kutatua tatizo la maji.
Tatizo la upatikanaji wa maji safi kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam limekuwa ni changamoto kubwa ambapo hadi sasa DAWASA ina uwezo wa kuzalisha lita milioni 300 kwa siku huku mahitaji yakiwa ni lita milioni 450
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top