Mwenyekiti
wa Taasisi ya Figo Tanzania Mh. Frederick Werema akizungumza na waandishi wa
habari leo jijini Dar es salaam kuhusu umuhimu wa kunywa maji safi na
salama kama moja ya njia za kukinga figo kuathiriwa na magonjwa mbalimbali na
kutoa wito kwa watanzania kuepuka tabia hatarishi kwa afya ya figo zikiwemo
za utumiaji wa pombe kupita kiasi, madawa ya kulevya, utumiaji wa dawa za
binadamu kupita kiasi na uvutaji wa sigara. Picha na Aron –
MAELEZO.
…………………………………………………………………..
Na.
Aron Msigwa – Dar es salaam.
Watanzania
wametakiwa kujenga tabia ya kuvitumia vituo vya afya kupima afya ya figo mara
kwa mara na kupata ushauri na tiba mapema pindi wanapogundulika kuwa na
matatatizo ya figo ili kuepuka kusababisha usugu wa ugonjwa
huo.
Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi ametoa kauli hiyo leo jijini
wakati akitoa tamko kuhusu maadhimisho ya Siku ya Afya duniani yatakayofanyika
tarehe 14 mwezi huu duniani kote.
Amesema
wananchi wengi wamekuwa wakichelewa kwenda kwenye vituo vya afya kuchunguza afya
ya figo zao kwa wakati ili kujua kama ni wazima au wameathirika ili
waweze kupata tiba sahihi ya ugonjwa huo.
Dkt.
Mwinyi amesema ugonjwa wa figo unazuilika na kutibika na kuongeza kuwa kinga ya
maradhi ya figo huanzia kwenye kaya na vituo vya awali vya utoaji wa huduma za
tiba na kuongeza kuwa maradhi haya yanawapata watu wengi hasa baadhi
ya vijana na watu ambao wamekua wakipata magonjwa ya kuambukiza kama vile
kuhara, Malaria, homa ya Ini, Pepopunda na Ukimwi.
Amesema
mwaka huu 2013 Tanzania inaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya
afya ya figo duniani kitaifa katika viwanja vya hospitali ya AICC Arusha kwa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na Chama cha Taifa cha Afya
ya Figo ikitoa elimu kuhusu umuhimu wa katika kudumisha afya ya figo kwa
kuongozwa na kauli mbiu isemayo ” Afya ya Figo kwa Maisha Bora: Epuka kuharibu
Figo”
Amefafanua kuwa lengo kuu
la kauli mbiu hiyo ni kuwahimiza wananchi kufahamu umuhimu mkubwa wa kiungo
hicho katika mwili wa binadamu.
”
Napenda kuwaeleza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu inatuhimiza watu wote tufahamu
kuwa figo ni kiungo muhimu sana katika maumbile yetu hivyo hatuna budi kutunza
viungo hivi katika miili yetu visije kupata madhara yoyote yanayoweza kujitokeza
kuviharibu” Amesema Dkt. Mwinyi.
Ameongeza
kuwa serikali ya Tanzania inafanya kila linalowezekana kuhakikisha kuwa fedha,
vifaa tiba na dawa za kukabiliana na ugonjwa huo zinapatikana ili kuinua na
kulinda afya ya jamii.
Katika
hatua nyingine Dkt. Mwinyi amesema maadhimisho ya mwaka huu yataambatana na
upimaji wa afya ya figo bure na kuongeza kuwa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii,
Taasisi ya Figo Tanzania na Kampuni ya Simu za mkononi ya Tigo Tanzania na Uhuru
One kwa pamoja watazindua programu ya kutuma ujumbe mfupi wa simu (sms) wa IJUE
AFYA YA FIGO YAKO”
Amesema huduma hiyo itatoa
fursa kwa wananchi kupata na kutuma taarifa zinazohusu hali zao za afya ambapo
wataweza kupewa maelezo na namna ya kupata huduma katika vituo mbalimbali vya
afya kwa kuanza na mkoa wa Dar es salaam, Zanzbar na baadaye kusambaa nchi nzima
ili kuwawezesha wananchi kuzifahamu afya zao kupitia simu zao za
mkononi.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Taifa ya Figo Tanzania ambaye pia ni
Mwanansheria mkuu wa Serikali Frederick Werema amesema kuwa tatizo la ugonjwa wa
figo nchini tanzania limekua likiongezeka kutokana na wananchi walio wengi
kushindwa kufuata kanuni za afya na kuzingatia lishe
bora.
Amesema kuwa
ugonjwa wa figo unazuilika endapo watu watajenga tabia ya kuepuka matumizi ya
baadhi ya dawa zenye athari kwa mwili wa binadamu, ulevi kupita kiasi, uvutaji
wa sigara, kula vyakula visivyofaa ama vyenye sumu na kuzingatia unywaji wa maji
safi na salama mara kwa mara.
Naye
Katibu wa Taasisi ya Figo Tanzania Dkt. Linda Ezekiel amefafanua kuwa idadi ya
wagonjwa wa figo nchini imekua ikiongezeka mwaka hadi mwaka na kufafanua kuwa
kati ya wagonjwa 1000 wanaohudhuria kwenye vituo vya afya kwa ajili ya matibabu
asilimia 3-9 wanasumbuliwa na matatizo ya figo huku akitoa wito kwa wananchi
kupima afya zao mara kwa mara.
Post a Comment