1. Kibanda leo ameingizwa theater ili kuanza
kufanyiwa upasuaji na kujengwa sura baada ya kupungua kwa majeraha na uvimbe
vilivyokuwa katika sehemu mbalimbali za mwili wake, hususan kichwani na
usoni.
2. Upasuaji huo
unazingatia matokeo ya uchunguzi ulifanywa kwa zaidi ya saa 48 na jopo la
madaktari na kubaini kwamba mbali na madhara ya awali, Kibanda pia aliumizwa
taya lake la kushoto.
3. Kuhusu jicho lake la
kushoto ambalo pia lilijeruhiwa, madaktari walisema wangetoa uamuzi kuhusu aina
ya upasuaji ambao wangeufanya baada ya kubaini hali halisi wakati watakapokuwa
wakijenga sura yake ambayo iliharibiwa kwa majeraha.
4. Wakati akipelekwa
theater ambako alikuwa akifanyia upasuaji ambao uliotarajiwa kuchukua saa zaidi
ya nne, alikuwa akilalamikia maumivu kutokana na kidonda kilichopo kwenye mguu
wake wa kushoto. Kidonda hicho pia ni matokeo ya unyama
aliyofayiwa.
5. Jana Rais Jakaya
Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana ambao wako Afrika Kusini
kikazi, walimtembelea Kibanda hosipitalini kumjulia hali. Rais Kikwete alisema
Serikali inajitahidi kuwasaka wahusika wa tukio la utesaji wa Kibanda na kwamba
wakikamatwa watafikishwa mahakamani.
Tutaendelea
kufahamishana kila hatua ya tiba ya Mwenyekiti wetu, na tunaomba tuendelee
kumwombea ili apone haraka.
--
Neville C. Meena,
Secretary General,
Tanzania Editors Forum - TEF,
Dar es Salaam - Tanzania.
Cell: +255 - 787 - 675555
+255 - 753 -
555556
Post a Comment