FIFA
YAWASILISHA MAREKEBISHO10
YA KATIBA KWA WARAKA
Shirikisho
la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limetuma mapendekezo 10 ya marekebisho ya
Katiba yake kwa wanachama wake kwa njia ya waraka.
Mapendekezo
hayo yametumwa kwa kila nchi mwanachama kupitia waraka namba 1320, ambapo
wanachama kwa kupitia kwa mashirikisho yao ya mabara watapiga kura ya ndiyo au
hapa. Kwa upande wa Afrika, wanachama wa FIFA wanatakiwa kuwasilisha kura zao
kupitia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF).
Baadhi
ya mapendekezo hayo ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji kuthibitishwa na Mkutano
Mkuu wa FIFA (FIFA Congress). Makamu wa Rais wa FIFA na wajumbe wa Kamati ya
Utendaji wanaochaguliwa katika mabara ambapo itabidi wathibitishwe na FIFA
Congress.
Muundo
wa Kamati ya Utendaji; nafasi moja ya vyama vya mpira wa miguu vya Uingereza
(British FAs) sasa inahamishiwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Ulaya (UEFA). Pia
Mwenyekiti wa Kamati ya Ukaguzi ya FIFA anatakiwa kushiriki vikao vya Kamati ya
Utendaji bila kuwa na haki ya kupiga kura.
Uchaguzi
wa Rais; mgombea anatakiwa kuungwa mkono na idadi ya kutosha ya vyama wanachama
kutoka katika mabara mawili tofauti. Ukomo wa uongozi; kuanzisha vipindi vya
uongozi. Ukomo wa umri; ukomo wa umri usiozidi miaka 72 wakati wa kugombea
utekelezwe.
Uwakilishi
wa kutosha kwa makundi yenye maslahi katika FIFA; makundi yenye maslahi katika
mpira wa miguu kama wachezaji wapate uwakilishi katika Kamati ya Mpira wa Miguu.
Uteuzi wa mwenyeji wa Fainali za Kombe la Dunia; uteuzi sasa ufanywe na Mkutano
Mkuu wa TFF.
WATAZAMAJI
13,398 WAZISHUHUDIA YANGA, KAGERA
Watazamaji
13,398 wameshuhudia pambano la Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kati ya Yanga na Kagera
Sugar lililochezwa juzi (Februari 27 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam
na kuingiza sh. 77,117,000.
Mechi
hiyo namba 130 iliyochezeshwa na Simon Mberwa kutoka mkoani Pwani ilimalizika
kwa Yanga ambao wanaongoza VPL wakiwa na pointi 42 kuibuka na ushindi wa bao 1-0
lililofungwa dakika ya 45 na Haruna Niyonzima.
Viingilio
vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata
mgawo wa sh. 18,291,297.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa
ni sh. 11,763,610.17.
Kiingilio
cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo waliokata tiketi hizo
walikuwa 11,908 na kuingiza sh. 59,540,000 wakati idadi ndogo ya washabiki
ilikuwa ya kiingilio cha sh. 20,000 kilichovutia washabiki 80 na kuingiza sh.
1,600,000.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 9,300,659.97, tiketi sh.
3,348,990, gharama za mechi sh. 5,580,395.98, Kamati ya Ligi sh. 5,580,395.98,
Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 2,790,197.99 na Chama cha Mpira
wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 2,170,153.99.
POLISI
KUIKABILI OLJORO KUNG’ANG’ANIA VPL
Polisi
Morogoro inaikaribisha Oljoro JKT ya Arusha kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini
Morogoro katika mechi pekee ya Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa
Tanzania Bara itakayochezwa kesho (Machi 2 mwaka huu).
Hata
hivyo, timu hizo haziko katika kinyang’anyiro cha kuwania ubingwa ambapo Yanga
ndiyo inayoongoza ligi hiyo ikiwa na pointi 42 wakati Oljoro JKT inayofunzwa na
Alex Mwamgaya ikiwa nazo 21 na Polisi Morogoro pointi 15.
Oljoro
JKT iko katika nafasi ya tisa. Polisi Morogoro ambayo katika mzunguko wa pili
imebadilika ikiwa chini ya Kocha Adolf Rishard inashika nafasi ya 12 ikiziacha
mkiani Toto Africans yenye pointi 14 na African Lyon ambayo ina pointi
13.
Ligi
hiyo itaendelea Jumatano (Machi 6 mwaka huu) kwa mechi kati ya Oljoro JKT vs
Tanzania Prisons (Sheikh Kaluta Amri Abeid), African Lyon vs Ruvu Shooting (Azam
Complex, Chamazi) na Mgambo Shooting vs Mtibwa Sugar (Mkwakwani) wakati Machi 7
mwaka huu ni JKT Ruvu vs Kagera Sugar (Azam Complex,
Chamazi).
Machi 9
mwaka huu kutakuwa na mechi mbili; Yanga vs Toto Africans 9Uwanja wa Taifa), na
Azam vs Polisi Morogoro (Azam Complex, Chamazi).
VILLA
SQUAD KUIVAA ASHANTI UNITED FDL
Michuano
ya Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea kesho (Machi 2 mwaka huu) katika
makundi yote matatu. Villa Squad itaivaa Ashanti United kwenye Uwanja wa Karume,
Dar es Salaam katika moja ya mechi za kundi B.
Kundi A
ni mechi kati ya Kurugenzi ya Mafinga dhidi ya Mbeya City wakati Polisi Iringa
vs JKT Mlale, na Majimaji vs Mkamba Rangers zilizokuwa zicheze kesho (Machi 2
mwaka huu), sasa zitaumana Machi 3 mwaka huu mjini Iringa na mjini
Songea.
Pia
kundi B kesho (Machi 2 mwaka huu) ni Green Warriors vs Transit Camp (Mlandizi)
wakati keshokutwa (Machi 3 mwaka huu) Polisi Dar vs Tessema (Karume) na Ndanda
vs Moro United katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini
Mtwara.
Mechi za
kundi C kesho ni JKT Kanembwa vs Polisi Tabora (Lake Tanganyika), Polisi Mara vs
Polisi Dodoma (Karume, Musoma), Morani vs Pamba (Kiteto) na Mwadui vs Rhino
Rangers (Kambarage,
Shinyanga)
Post a Comment