*LIGI YA VODACOM KUENDELEA J’MOSI
Ligi
Kuu ya Vodacom (VPL) kuwania ubingwa wa Tanzania Bara inaendelea
Jumamosi (Machi 16, 2013) kwa mechi tatu zitakazochezwa katika miji ya
Mwanza, Dar es Salaam na Manungu, Turiani mkoani Morogoro.
Toto
Africans inayopigana kukwepa kurudi daraja la kwanza itakuwa mwenyeji
wa Mgambo Shooting kutoka Tanga katika mechi itakayochezwa Uwanja wa CCM
Kirumba.
Vinara
wa ligi hiyo Yanga wataumana na Ruvu Shooting kwenye Uwanja wa Taifa
wakati Uwanja wa Manungu utakuwa mwenyeji wa mechi ya Mtibwa Sugar na
Coastal Union.
*UCHAGUZI TAFCA KUFANYIKA MOROGORO
Uchaguzi
wa viongozi wa Chama cha Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA)
utafanyika Jumamosi (Machi 16 mwaka huu) mjini Dodoma ambapo wajumbe
wanatakiwa kuripoti siku moja kabla ya uchaguzi.
Wagombea
waliopitishwa kuwania uongozi na Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA chini ya
uenyekiti wa Ramadhan Mambosasa ni Oscar Don Koroso (Mwenyekiti), Lister
Manyara (Makamu Mwenyekiti) na Katibu (Michael Bundala).
Wengine
ni Gabriel Gunda (Katibu Msaidizi), Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania- TFF (Wilfred Kidao) wakati
wagombea ujumbe wa Kamati ya Utendaji ni Jemedali Saidi, George Komba na
Magoma Rugora.
*KIM KUTAJA KIKOSI CHA KUIKABILI MOROCCO
Kocha
Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen anatarajia
kesho (Machi 13 mwaka huu) kutaja kikosi chake kitakachoivaa Morocco.
Mkutano
huo wa Waandishi wa Habari utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ofisi za
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Taifa Stars inayodhaminiwa
na Kilimanjaro Premium Lager itacheza na Morocco kwenye Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam, Machi 24 mwaka huu.
Mechi
ya Ligi Kuu ya Vodacom kati ya Simba na Coastal Union iliyochezwa juzi
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam imeingiza sh. 36,820,000 kutoka na
watazamaji 6,284.
Viingilio
katika mechi hiyo namba 138 iliyomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi
wa mabao 2-1 vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000
huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 8,265,752.45 wakati Kodi ya
Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 5,616,610.17.
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 4,202,924.97,
tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 2,521,754.98, Kamati ya Ligi
sh. 2,521,754.98, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
1,260,877.49 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 980,682.49.
Post a Comment