Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh.
Pereira Silima akikabithi mfano wa hundi
ya shilingi millioni moja kwa captain wa timu ya Mbezi Ally Shila Kulola baada
ya timu yake kuibuka washindi wakwanza wa michuano ya mpinga Cup kwa kushinda
Makondeko mabao 7-6
Afisa uhusiano wa Airtel Jane Matinde
akikabithi zawadi kwa captain wa timu ya makondeko Stanley Peter mara baada ya
kuibuka washindi wa pili wa mashindanoo ya mpinga Cup yaliyohusisha waendasha
pikipiki (bodaboda) kwa muda wa wiki moja katika viwanja vya oyesterbay polisi.
Kushoto pembeni ni kiongozi wa timu ya makondeko bwana Mneke S Mneke
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP.
Mohamed Mpinga akibadilishana mawazo na Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh.
Pereira
Silima ambaye wakati wa fainali za michuano ya mpinga Cup
iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.
Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani SACP.
Mohamed Mpinga akimtambulisha Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh.
Pereira Silima ambaye ni mgen rasmi wakati wa fainali za michuano ya mpinga
Cup iliyofanyika jana katika viwanja vya oyesterbay police.
...........................................................................................................
Michuano ya mpinga Cup imemalizika rasmi jana
baada ya mchezo wa fainali thidi ya timu ya Mbezi na makondeko ambapo, timu
hizo zilitoka sare ya bao 2 -2 na kuingia kwenye mkwaju wa penalti ambapo timu
ya kawe iliibuka na ushindi wa mabao 7 -6
Katika michuano hiyo iliyodumu kwa muda wa
wiki nzima na kushirikisha timu nane kutoka katika mkoa wa kipolisi wa kinondoni
timu ya mikocheni Iliibuka kuwa mshindi wa tatu wa michuano
hiyo.
Akiongea wakati wa kufunga michuano hiyo
mgeni rasmi Naibu waziri wa mambo ya ndani Mh. Pereira Silima alisema” tunawashukuru waandalizi wa
michuano hii na wadhamini ambao ni Airtel, Mr price, home shoping center na
Rotary Club Dar es Saalam kwa ushirikiano wao mkubwa na mchangao wao katika
kuhakikiksha mashindano haya yanafanyika kwa mafanikio. Hii nijitahada ya pekee
kuunganisha michezo na elimu ya usalama barabarani.
Tumegundua vipaji vingi hapa tunawaasa
wachezaji hawa wajiendeleze mbali na kuendesha pikipiki kwa muda wa ziada
wataweza kucheza mpira na kupata njia nyingine ya kipato kwa michezo ni
ajira.
Naye Mkuu wa kikosi cha Usalama barabarani
SACP. Mohamed Mpinga amewashukuru washiriki wote wa michuano hii na kusisitiza
wananchi na watanzania kwa ujumla kutii sheria bila
shurutishi.
Akiongea kwa niaba ya wadhamini Afisa
Uhusiano wa Airtel Jane Matinde alisema” mashindano haya yamekuwa ya mvuto
mkubwa kwa washiriki na wadau wa michezo zaidi tumeshuhudia jinsi mafunzo ya
elimu ya usalama barabarani yalivyoendesha na kuelimisha watumiaji wa barabara
waliokuwa wakihudhuria hapa.
Tunaamini kuendelea na juhudi hizi tutaweza
kupunguza idadi za ajali barabarani. Airtel tunaahidi kuendelea kushirikiana na
jeshi la polisi usalama barabarani katika shughuli mbalimbali za uelimishaji
umma juu ya sheria za barabarani
Michuano ya mpinga cup kwa wilaya ya
kinondoni imefika tamati hapo jana na mpango ni kuwa na michuano hii pia katika
mkoa wa ilala na temeke na kisha kuendelea na michuano hii nchini nzima.
Mwisho
Post a Comment