Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

UNAMKUMBUKA BIBI WA MIAKA 61 ALIYEUA JAMBAZI KULE BAGAMOYO?HII NDIO TAARIFA MPYA

 

Hapa ndio bibi alisimama na kupiga risasi ilitoboa huo mlango wa mbao na kumpata jambazi aliekua nje akijaribu kuvunja mlango.
Hii post ni maalum kuhusu taarifa za uhakika kuhusu yule bibi wa miaka 61 aliyeua jambazi kwa risasi Bagamoyo Pwani December 2012.
Stori za kuaminika ni kwamba bibi huyu ambae anamiliki shule mbili, amekimbia nyumbani kwake na sasa hajulikani alipo, hiyo imetokana na vitisho vilivyomuandama.
Siku kadhaa baada ya kufanikiwa kuua jambazi mmoja kati ya majambazi zaidi ya watano waliomvamia nyumbani kwake, Bibi alisafiri kwenda nje ya nchi kwa matibabu lakini kabla ya kurudi nyumbani alipata taarifa za kushtua.
Hapa ndio kwa bibi Mwajuma Said Marwa Masaigana ambae anatimiza umri wa miaka 62 May 2013.
Uhakika wa hizo taarifa ulionyesha kwamba kundi la watu wasiojulikana wakiwa na silaha wamekua wakimuwinda wakiwa na silaha.
Bibi sasa hivi hapatikani kwenye simu, ameicha nyumba yake ya ghorofa ufukweni mwa bahari ya hindi na sasa anaishi kusikojulikana, ni bibi shupavu ambae uhodari wake wa kutumia bastola kwa uzoefu wa mwaka mmoja jeshini ndio ulimfanya aue jambazi moja kati ya majambazi zaidi ya matano yayovamia nyumbani kwake December 2012, ni nyumba ya ghorofa.. na chumba cha bibi chenye sebule yake pia kiko juu na ngazi ziko nje, hakuna ngazi ya ndani ndio maana ilikua rahisi majambazi kupanda walipoona mpango wa kurusha risasi wakiwa chini hauna nguvu.
.
Majambazi hao walitumwa kumuua yeye na hawakuiba mali japo walipovunja nyumba kwenye upande wa chini waliingia mpaka kwenye chumba ambacho ndio kilikua na mali zote zenye thamani lakini hawakuchukua chochote.
Kwa kipindi kirefu Bibi huyu alikua akitumiwa msg za vitisho, kupigiwa simu na namba asizozijua na mpaka kuvamiwa nyumbani kwake, siku chache tu baada ya jirani yake ambae ni mzungu kuvamiwa.
Viganja vyangu vinahusika sana wakati huu kumtafuta kamanda wa Polisi Pwani ili kujua walipofikia manake kuna taarifa kwamba Wananchi tayari walishatoa majina ya majambazi manake wanawafahamu.
millardayo.com
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top