***********
VITENDO vya
wanawake kufanya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea kutikisa Halmashauri
ya Manispaa ya Iringa mkoani Iringa baada ya mwanamke mmoja aliyefahamika kwa
jina la Monica au Chenzia (20) mzaliwa wa Mtera Iringa vijini anayedaiwa kuwa
ni mhudumu wa bar mjini Iringa kuzaaa mtoto wake kisha kumunyonga na kumtupa
porini.
Tukio hilo
limetokea leo jumapili katika eneo la Isoka katika Manispaa ya Iringa
.
Wakizungumza
na mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com wakazi wa Mwangata katika
Manispaa ya Iringa akiwemo aliyepata kuwa mshiriki wa mashindano ya Maisha
Plus Shauri Mnyinga maarufu kwa jina la mama Afrika alisema alisema kuwa baada
ya mwanamke huyo kutupa mtoto huyo wananchi waliamua kufanya msako mkali wa
kufuatilia michilizi ya damu hadi katika chumba cha mwanamke huyo na kumkuta
akiwa ndani amelala.
Imeelezwa
kuwa mwanamke huyo anafanya kazi katika bar mmoja maarufu iliyopo Mlandege
katika Manispaa ya Iringa alitoa mimba hiyo kwa kutumia dawa aina ya
Mistropastor na dawa hizo kwa kawaida haziuzwi kiholela kutoka na bei
yake kuwa kubwa kwa kidonge kimoja kuuzwa kwa Tsh
20,000.
Shauri
alisema kuwa kwa kipato cha mwanamke huyo kwa kazi hiyo ya bar ambapo
mshahara wake kwa ni kati ya 20,000 na 30,000 hadi amepata fedha za kutoa
mimba hiyo.
Hata hivyo
wengi wamekuwa wakijiuliza iwapo mwanamke huyo angepata UKIMWI angeweza
kuutoa .
Mwanamke huyo
amekamatwa na hadi sasa yupo chini ya vyombo vya dora na kuwa alikutwa akiwa
na damu mwili mzima baada ya kushindwa kuoga baada ya kutoa mimba
hiyo.
Kwa upande
wake mwanamke huyo alidai kuwa aliamua kutoa mimba hiyo baada ya kuona maisha
ni magumu na kati ya wanaume wote zaidi ya watano aliopata kuwa na mahusiano
nao hakuna hata mmoja ambae anakubali mimba hiyo hivyo kutokana na ukata wa
maisha amelazimika kutoa mimba hiyo .source francis
godwin

Post a Comment