Bibi
wa mwanafunzi Mwenjuma Magalu, Amina Mohamed (kulia) akizungumza na
Mhariri wa mtandao wa Thehabari, Joachim Mushi kijijini Msasa, wilayani
Handeni juzi.
Mwenjuma
Magalu (wa kwanza kulia mstari wa pili) ambaye kwa sasa ni mwanafunzi
wa kidato cha pili Shule ya Sekondari Komnyang’anyo akiwa darasani na
baadhi ya wanafunzi wenzake
Na Thehabari.com,
Handeni
UTAFITI wa
kihabari uliofanywa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA),
Machi 2012 umefanikisha kumrudisha shuleni mwanafunzi wa sekondari aliyekuwa
ametelekezwa yeye pamoja na familia yao.
Mwenjuma
Magalu ambaye kwa sasa ni mwanafunzi wa kidato cha pili katika Shule ya
Sekondari Komnyang’anyo alitelekezwa na babayake yeye pamoja na mamayake mwaka
jana, hivyo kushindwa kujiunga na kidato cha kwanza katika shule hiyo licha ya
kuchanguliwa kuendelea na masomo.
Hata hivyo
baada ya utafiti wa kihabari kufanyika kijijini Msasa Wilaya ya Handeni na
taarifa za mtoto huyo kushindwa kujiunga na sekondari baada ya mamayake (kwa
sasa marehemu) kukosa uwezo kuripotiwa, alijitokeza mfadhili wa kumsomesha
ambaye anagharamia masomo yake hadi sasa.
Akizungumza
na mwandishi wa habari hizi juzi akiwa shuleni. Komnyang’anyo, mwanafunzi huyo
aliishukuru TAMWA kwa kuibua tatizo la familia yao kwa umma na kupatikana kwa
mfadhili ambaye amemrudisha masomoni licha ya familia yao kutelekezwa.
“Binafsi
nawashukuru sana hao (TAMWA) waliopaza sauti hadi mjuu wangu kurudi shuleni…hii
kwetu ilikuwa ni ndoto kwetu maana mtoto mwenyewe alikuwa amekata tamaa kabisa
kurudi shuleni na alikuwa kaanza kufanya vibarua mitaani huku wenzake
wakiendelea na shule,” alisema bibi wa mtoto huyo, Amina Mohamed akizungumza.
Bibi huyo
akizungumzia maisha ya sasa ya familia hiyo alisema bado wanahitaji msaada wa
huduma hasa baada ya mwanaye kufariki dunia mwaka jana na kumuachia watoto
wake.
Aliongeza
kwa sasa yeye ni mgonjwa wa TB anayetumia dawa hivyo kwa hali yake ameshauriwa
kupumzika jambo ambalo limempa mzigo mkubwa kimajukumu mwanafunzi (Mwenjuma),
kufanya kazi za nymbani kama kupika kulima na shughuli nyingine.
Hata hivyo
mama wa mtoto huyo (Hadija Magalu) ambaye alitelekezwa na mzazi mwenzake alifariki dunia mwaka
jana kwa tatizo la uzazi na kuiacha tena familia hiyo ya watoto watatu katika
hali ngumu zaidi chini ya malezi ya bibi mzaa mama
Post a Comment