Waziri wa
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta
Na: Beatrice
Moses
Waziri wa Ushirikiano wa
Afrika Mashariki, Samuel Sitta amewajibu wabunge wa Afrika Mashariki akisema
wengi hawahudhurii vikao vya kupewa mwongozo kuhusu bunge hilo kwa kuwa
“wanataka kulipwa posho”. Kauli hiyo ya Sitta ambaye pia ni Mbunge wa Urambo
Mashariki, imekuja siku moja tangu wabunge hao waichongee wizara hiyo kwa Kamati
ya Bunge ya Mambo ya Nje, kwamba imeshindwa kuwapa mwongozo pale wanapokwenda
kwenye vikao vya Bunge la Afrika Mashariki. Akizungumza katika kikao cha kamati
hiyo jana, Sitta alisema wabunge hao wamekuwa vinara wa kuomba posho
kila
wanapotakiwa kuhudhuria
kwenye mikutano ya wizara yake.
Katika maelezo yake
Sitta alimeshutumu Katibu wa Wabunge hao, Shyrose Bhanji kuwa ndiye anayeongoza
kwa kutoa udhuru mara kadhaa, hivyo kutoudhuria vikao vinavyoitishwa na wizara
hiyo.
“ Wizara imejiwekea
utaratibu mzuri wa kukutana na wabunge hao, lakini nafikiri katibu wao ndiye
anayeongoza kwa kutohudhuria,” alisema Sitta na kuongeza:
“Nadhani amekuwa na
shughuli nyingi sana, tuna utaratibu wa kukutana kila baada ya miezi mitatu,
lakini ndiye aliyeongoza pia kutoa malalamiko hayo yasiyo na
ukweli.”
Waziri Sitta katika
majibu yake alifafanua kwamba wizara hiyo bado haijapewa majukumu rasmi ya kutoa
mwongozo kwa wabunge hao.
Mbali na Sitta, naibu
wake, Abdullah Juma Saddallah naye alieleza tabia za wabunge hao huku
akisisitiza kuwa posho kwao ndiyo jambo la umuhimu zaidi.
Saddallah alisema
malalamiko hayo ni ya ajabu na yamewashtua kwa sababu hayana ukweli, lakini
wamekuwa wakijikuta kwenye mtihani kwani kuna baadhi ya wabunge hao wakiitwa
kuudhuria vikao utambulia kuuliza posho.
“Wizara haina fungu la
kuwahudumia wabunge hao, hili limekiwishajadiliwa katika vikao vya kamati
vilivyopita na ilikubalika kuwa ofisi ya bunge itaangalia uwezekano wa kuwapatia
ofisi na vitendea kazi vingine,” alisema Saddallah.
Alisema pia kabla ya
kuteuliwa wabunge hao wizara hiyo kwa kushirikiana na ofisi ya Bunge ilifanya
uchambuzi na kuandaa mwongozo utakaowezesha ushirikiano na uwajibikaji baina ya
Bunge la Tanzania na wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki
(EALA).
“Mwongozo huu umewezesha
kuundwa kwa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa ambayo
awali ilitarajiwa kuwa Kamati ya Bunge ya Afrika Mashariki inayotoa nafasi ya
kutoa taarifa za utekelezaji na kupata mwongozo,” alisema Naibu Waziri
huyo.
Post a Comment