Mwenyekiti wa Tawla Aisha bade akisisitiza jambo wakati wa sherehe ya kuwapongeza wanachama wa tawla na kutoa tunzo kwa wanachama wa ambao wamefanikiwa kupata nafasi za juu na kuwa na mchango mkubwa kwa tawla na kuwa kioo au mfano kwa wanawake wengine.iliofanyika kwenye ukumbi wa JB BELMONT jijini Dar es salaam HABARI, PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE
SKYLIGHT BAND ikitoa burudani wakati wa sherehe ya kuwapongeza wanachama wa tawla na kutoa tunzo, wakwanza (kushoto) MARY LUKAS,(wapili kulia) ANETH KUSHABA , SAM MACHOZI, SONI MASAMBA, ALLAN KISO SOLO,
Afisa Mradi Kitengo cha Ardhi Tawla. Latifa Mwabondo (kushoto)akiwa kwenye picha ya pamoja na. Ashura Mzava.wakati wa sherehe ya kuwapongeza wanachama wa tawla.
Mkuu wa Kitengo cha Utafiti na Uenezi wa Tawla, Nasieku Kisambu wakwanza kushoto) Afisa Mradi Kitengo cha Ardhi Tawla. Latifa Mwabondo (kulia) Afisa ufuatiliaji na Tathimini Juma Mwenga (katikani)wakiteta jambo wakati wa sherehe ya kuwapongeza wanachama wa tawla.
Sasa ni wakaa kwenda mbele ti wa burudani kwkama wanavyoonekana katika picha
Dk Hellen Kijo-Bisimba alisema changamoto bado ni kubwa na hasa katika sehemu za vijijini ambapo wanafuata mila zaidi na inaaminika mwanamke hatakiwi kumiliki ardhi.
LICHA ya kuwepo kwa fursa za wazi za kisheria za kuwawezesha wanawake kumiliki ardhi, imeelezwa kuwa bado umiliki wa ardhi ni mdogo kwao.
Kauli hiyo imeelezwa na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angela Kairuki wakati wa semina ya chama cha wanasheria wanawake (Tawla) ya umiliki wa ardhi kwa wanawake na uwekezaji iliyofanyika jana jijini Dar es Salaam.
Waziri Kairuki alisema kutokana na muamko mdogo uliopo kwa wanawake kumiliki ardhi kswa kiasi kikubwa kinawafanya washindwe kutumia fursa za kisheria za kuwawezesha kumiliki ardhi.
“Fursa ziko wazi kuwa kila mtu ana haki ya kumiliki ardhi lakini baadhi ya wanawake hawajitokezi, wakumbuke ardhi ni dhamana kubwa ambayo hata kama unafanya biashara unaweza ukaitumia kuombea mikopo” alisena Waziri Kairuki.
Naye Mwenyekiti wa Tawla Aisha bade alisema chama chake kimekuwa kikijitahidi kufanya ushawishi kwa kutoa elimu kuhusiana na sula la umiliki wa ardhi kwa wanawake.
Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa kituo cha sheria na Haki za Binadamu(LHRC)
Post a Comment