Na Ali Issa Maelezo Zanzibar
Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imetangaza rasmi, kuazia leo Matangazo ya dijital ya takuwa hewani kutoa huduma zake kwa majaribio ili kuona wananchi watao pata ving’amuzi wana faidika na huduma hiyo muhimu ya matangazo.
Amesema matangazo hayo ya taenda hewani baada ya kukamilika miundo mbinu ya kufanikisha urushaji wa mangazo ya dijital na yale matangazo ya analog yataendelea kuwepo mpaka wana nchi walio wengi kuweza kumiliki vingamuzi na ndipo serikali kutangaza kuyafunga mangazo ya analojia.
Hayo yamesemwa leo huko Hoteli ya Bwawani na Waziri wa Habari Utalii,Utamaduni na Michezo Saidi Ali Mbaruok wakati wa uzinduzi wa matangazo ya dijital na upatikanaji wa ving’amuzi mbele ya waandishi wa habari walio fika Hotelini hapo.
Amesema matangazo hayo yako tayari kurushwa hewani leo kwamajaribio baada ya kukamilika miundo mbinu ya matangazo ambapo kwa ujumla miundo mbinu hiyo inamilikiwa na serikali na wateja wao kwa sasa walio nunua vingamuzi , watakuwa wana ipata huduma hiyo bila pingamizi yoyote.
“wananchi wa Zanzíbar walishamiliki miundo mbinu ya digital ,jambo ambalo ni lakujivunia sana kwani karibu nchi zote jirani miundo mbinu yao ya dijitali inamilikiwa na kampuni kutoka nje ,sisi Zanzíbar miundo mbinu yetu ya dijitali ni mali ya serikali ya Zanzíbar.alisema waziri.
Aidha waziri huyo alisema kuwa matangazo hayo yataruka yakiwa chini ya utalaamu wa kamuni ya Agape kwa muda wa miaka miwili kwa masharti walioekeana na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzíbar, huku ikiwafundisha watalamu wazalendo na mna ya kuitumia mitambo hiyo ya kisasa pamoja na uendeshaji vipindi vilivyo kubaliwa na serikalini yao.
“Serikali imetiliana mkataba wa uendeshaji wa miundo mbinu wa miaka miwili na kampuni ya Ágape katika kipindi hicho cha miaka miwili kampuni ya Ágape itaendesha mitambo hiyo kwa masharti atayo pewa na serikali yetu na wakati huo huo wakiwafundisha wataaalamu wetu ili baada ya muda huo kumalizika wataalamu wetu wa weze kuindesha wenyewe. Alisema waziri.
Waziri huyo alisema kuwa wana nchi wasihamanike juu ya bei ya kingamuzi ni ileile ya shilingi elfu hamsini 50000 ambayo ni rahisi kwani ilizingatia halizao , ispokuwa kilicho ongezeka ni gharama za usajili shilingi 1500 na shilingi 8000 ni malipo ya awali ya mwezi kituambacho ni cha kawaida.
Serikali imekusudia kuleta vingamuzi laki tatu 300000 ifikapo mwezi wa tatu mwaka huu lakini kwa sasa jumla ya vingamuzi 5000 tayari vimeshawasili zanzbar natayari kuzwa katika maeneo yalio sajiliwa ikiwemo raha leo Studio.
Imetolewa na Idara ya Habari Maelezo Zanzíbar.
Post a Comment