Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akionyeshwa vifaa vya
kufungia samaki kabla ya kusafirishwa nje ya nchi na meneja udhibiti ubora wa
kiwanda cha samaki cha Vicfish mjini Mwanza Bw Jacob Maiseli.
Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Charles Kitwanga akipata Maelezo ya Utengenezaji
wa Samaki na Meneja udhibiti ubora wa kiwanda cha samaki cha Vicfish Bw Jacob
Maiseli wakati wa Ziara ya kutembelea na kukagua Uchafuzi wa Mazingira JIjini
Mwanza.


…………………………………………………………
Evelyn
Mkokoi
Story Mazingira
Mwanza
Uelelwa mdogo kwa wananchi
juu ya suala zima la uhifadhi na usimamazi wa mazingira, imeelezwa kuwa ni moja
ya changamoto ya usimamiz wa mazingira katika jiji la mwanza. Hayo yameelezwa
leo na Afisa Mazingira wa mkoa mwa Bw. Charles Amani wakati akiota taarifa kwa
naibu wazir Ofisi ya Makamu wa Rais katika Ziara ya kutembelea viwanda mjini
Mwanza.
Pamoja na changamoto hiyo
mkoa pia unakabilina na upungufu wa vifaa vya udhibiti wa taka ngumu na
kutokuwepo kwa teknolojia ya ufuatiliaji wa uchafuzi wa mazingira kwa hewa
kutoka viwandani na kwenye magari pamoja na kutokuwa na dampo la
kisasa.
Bw. Amani maeeleza kuwa
pamoja na changamoto hizo, jiji la mwanza limekuwa likiongoza kwa usafi wa
mazingira kwa kipindi cha miaka saba mfululizo, kutekelezaji wa kampeni ya
upandaji miti pamoja na miradi mbali mbali ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia
nchi kwa kushirikiana na sekta binafsi.
Kwa upande wake Naibu
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mh. Charles Kitwanga ameeleza kuwa lengo la
ziara yake mkoani Mwanza si kufungia viwanda bali ni kutaka kuwa na msimamo wa
pamoja na kuzingatia na kutekeleza sheria ya usimamizi wa mazingira, ili iwe
yenye manufaa kwa watanzania, “lengo la kuja ni kuhakikisha sheria inafuatwa”
alisisitiza.
Mh. Waziri aliongeza kwa
kusema kusema kuwa ni vyema Halmashauri na wizara husika zikajipanga ili kuona
namna ya kuwapatia sehemu mbadala wananchi wanaoishi milimani bila kuwabugudhi,
ili kule nako kupangwe ili kuwe na mazingira endelevu.
Wakati huohuo, kamanda wa
police wa kikosi maalum cha mazingira Nchini Bw. George Mayunga ameeleza kuwa
jeshi la police lipo tayari kupambana na wahalifu wa mazingira,ili kujenga
mazingira endelevu.
Post a Comment