Mhe. Waziri Mkuu wa Denmark akiwa amefuatana na Mhe.
Mary Nagu (Mb.), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji
pamoja na Mhe. Magesa Mulongo, Mkuu wa Mkoa wa Arusha mara baada yakuwasili
mkoani Arusha akitokea Dar es Salaam
Mhe. Thorning-Schmidt akilakiwa kwa shangwe na
baadhi ya kina mama wa Mkoa wa Arusha
Waziri Mkuu wa Denmark, Mhe. Helle Thorning-Schmidt
akisalimiana na viongozi mbalimbali wa Mkoa wa Arusha mara baada ya kuwasili
katika Uwanja wa Ndege wa Mkoa huo akitokea Dar es Salaam. Mhe. Thorning-Schmidt
yupo nchini kwa ziara ya siku nne kauanzia tarehe 5 hadi 8 Machi,
2013.
Mhe. Thorning-Schmidt akilakiwa kwa shangwe na baadhi
ya kina mama wa Mkoa wa Arusha
Mhe. Thorning-Schmidt pamoja na wenyeji wake
wakifurahia burudani kutoka moja ya kikundi cha ngoma ya Kimasaai iliyokuwepo
Uwanjani hapo wakati wa mapokezi.
Mhe. Waziri Mkuu wa Denmark kwa pamoja na Mhe. Waziri
Nagu na Mkuu wa Mkoa wa Arusha wakipata picha ya pamoja na kikundi cha ngoma
wakati wa mapokezi yake Arusha
Mhe. Thorning-Schmidt akisaini Kitabu cha Wageni mara
baada ya kuwasili katika Mahakama ya Kimataifa ya Mauaji ya Kimbari ya Rwanda
(ICTR) iliyopo Jijini Arusha
Mhe. Thorning-Schmidt akizungumza na uongozi wa
Mahakama ya ICTR (hawapo pichani) mara baada kupokea taarifa kuhusu utendaji wa
mahakama hiyo.
Rais wa Mahakama ya ICTR, Mhe. Jaji Vagn Joensen
akitoa taarifa fupi ya utendaji wa Mahakama hiyo kwa Mhe. Thorning-Schmidt
(hayupo pichani)
Mhe. Thorning-Schmidt akiwa katika picha ya pamoja na
uongozi wa Mahakama ya ICTR mara baada ya mazungumzo nao. Wengine katika picha
ni Mhe. Waziri Nagu (watatu kutoka kulia), Mhe. Mulongo (mwenye tai nyekundu) na
Bw. Jacob Msekwa (kulia), Mwakilishi wa Balozi wa Tanzania katika nchi za Nordic
ikiwemo Denmark.
Mhe. Waziri Mkuu, Thorning-Schmidt akisaini kitabu cha
wageni alipowasili kijijini Lepurko
Mhe. Waziri Mkuu, Thorning-Schmidt akivalishwa Vazi
Rasmi linalovaliwa na kina mama wa Kimasai mara baada ya kuwasili katika Kijiji
cha Wamaasai cha Lepurko kilichopo Wilayani Monduli.
Moja ya nyumba maarufu kama "Boma" zilizopo kijijini
hapo
Mhe, Thorning-Schmidt akitoka ndani ya nyumba "Boma"
aliyoitembelea kijijini hapo.
Mhe. Thorning-Schmidt akihutubia wananchi (hawapo
pichani) wa Kijiji cha Lepurko
Mhe. Thorning-Schmidt akiagana na Waziri Mkuu Mstaafu
na Mbunge wa Monduli, Mhe. Edward Lowassa mara baada ya kuhitimisha ziara yake
katika kijiji cha Lepurko.
Mhe. Thorning-Schmidt akiangalia bidhaa mbalimbali
zinazotengenezwa kwa shanga na kina mama wa kijijini hapo
Moja ya shughuli maalum iliyompeleka Mhe.
Thorning-Schmidt kijijini Lepurko ni kuzungumza na kina mama na kusikiliza
matatizo na changamoto mbalimbali wanazokutana nazo katika maisha yao ya kila
siku kama anavyoonekana.
Sehemu ya Wananchi wa Kijiji cha Lepurko wakisikiliza
kwa makini hotuba ya Mhe. Thorning-Shmidt (hayupo pichani) ambapo aliahidi
kuwasaidia katika kutatua tatizo la upatikanaji wa maji safi na salama.Picha
zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
Post a Comment