Naibu Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo
Mulugo akizindua tovuti ya www.shuledirect.co.tz itakayosaidia
kuboresha utoaji wa huduma za elimu hapa nchini. Uzinduzi huo ulifanyika jijini
Dar es Salaam. (Picha na Habari Mseto Blog)
DAR ES
SALAAM, Tanzania
NAIBU
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Philipo Mulugo, amerudisha adhabu ya
viboko kwa wanafunzi wa shule zote ili kurudisha nidhamu iliyotoweka kwa
wanafunzi.
Mbali na
adhabu hiyo kurejea Mulugo pia amewataka walimu kuwanyang’anya simu wanafunzi
watakaokutwa nazo kwani zinachangia kumomonyoa kiwango cha elimu kwa utumiaji wa
facebook.
Akizungumza jijini Dar es salaam wakati wa utambulisho
wa mfumo wa www.shuledirect.co.tz utakaosaidia kuboresha utoaji wa huduma za elimu
nchini, Mulugo alisema kuwa ni jukumu la kila mwanajamii kushirikiana na
Serikali katika kutatua changamoto zinazoikabili sekta ya elimu
nchini.
Mulugo
alisema kuwa japo karne hii ni sayansi, teknolojia na utandawazi ni vyema
kuwahimiza wanafunzi kutumia mitandao katika kutafuta maarifa na kusoma tafiti
mbalimbali kwa kuzingatia mila na desturi.
Pia alisema
kuwa mfumo huo utasaidia wanafunzi, walimu na jamii nzima katika kuongeza
ufahamu wenye tija katika kuchochoea maendeleo
yataaluma.
Naye
Mwanzilishi wa program hiyo, Faraja Nyalandu, alisema kuwa mpango huo ili
malengo ya elimu bora yafikiwe ni muhimu kila mtu atimize wajibu
wake.
Nyalandu
alisema kuwa Mpango huo ni mfumo wa kuweza kujisomea katika mtandao kwaajili ya
wanafunzi wa sekondari.
Alisema
kuwa malengo ya mfumo huo ni kumuwezesha mwanafunzi kujisomea, kufanya mazoezi,
kufahamu mtiririko wa anachopaswa kujifunza kupitia mtaala wa kuweza kushiriki
katika majadiliano ya kiakademia.
Post a Comment