HAPA AKITEMA MAPOVU HUKU
AKISEMA ANA NJAA SANA.
WAZEE WANAOSADIIWA KUWA NI
WACHAWI WAKIWA CHINI YA ULINZI KITUO CHA POLISI,KUTOKA KUSHOTO NI MWAJUMA MPONI
(70) NA KULIA NI SHIJA NKWABI (80)
Watu wawili wamenusurika
kuuwawa usiku wa kuamkia juzi katika kijiji cha Mhongolo wilaya ya kahama mkoani
shinyanga, baada ya kukutwa katika mazingira yanayodaiwa kuwa ya
kishirikina.
Watu hao
waliojitambulisha kwa majina ya Mwajuma Mponi (70) wa Nduku, na Shija Nkwabi(80)
wa Nyashimbi wilayani humo, wameanguka kijijini hapo wakitokea kijiji cha nduku
wiyani humo wakielekea Nyihogo Kahama kwa shughuli za
kishirikina.
Katika maelezo yao wazee
hao wamedai kuwa wameanguka baada ya kutokea ajali ya kishirikina huko angani,
ambapo waligongana na wenzao ambao hawakuwafahamu walikotoka na walikokuwa
wanaelekea.
Sambamba na hayo imeelezwa
kuwa wazee hao walikuwa uchi wakati wakianguka kabla ya kusaidiwa nguo na mama
mmoja wa maeneo ya Kafe Latino barabara ya Mhongolo.
Jeshi la Polisi la
Wilayani humo likiri kutokeakwa jambo jambo hilo na kwamba uchunguzi bado
unaendelea na taarifa zitatolewa baadaye.
WAZEE WAKIWA HOI,HUKU WA
KUSHOTO AKIWA ANATEMA MATE OVYO KITUONI HAPO.
BIBI AKIWA AKIWA HOI BAADA
YA KUDONDOKA USIKU WA LEO
HAPA BIBI AKISAIDIWA
KUINUKA BABADA YA KUVALISHWA NGUO NA WASALIMIA WEMA.
ASKARI POLISI WAKIWASAIDIA
KUWAPANDISHA KWENYE GARI.
HAPA WAKIPELEKWA KITUO CHA
POLISI
MWANDISHI WA HABARI WA
GAZETI LA MAJIRA PATRICK MABULA AKICHUKUA MAELEZO TOKA KWA MASHUHUDA
WALIOSHUHUDIA TUKIO HILO.
HAPA NDIPO ENEO AMBALO
WACHAWI HAO WALIPODONDOKEA.
Post a Comment